1Katibu Mkuu wa WMO Prof
Petteri Taalas katika picha ya pamoja na menejimenti ya TMA.
SHIRIKA la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization (WMO)) ni taasisi mahsusi la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya ushirikiano wa kimataifa yanayohusiana na ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na namna mifumo hii inavyoathiri mazingira yetu. Shirika hufanya kazi zake kupitia taasisi za hali ya hewa za nchi wanachama (National Meteorolgical and Hydrological Services - NMHSs) ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni mwakilishi rasmi wa shirika hili hapa nchini.
Katibu Mkuu wa WMO
amefanya ziara katika ofisi za TMA ili kujionea shughuli za hali ya hewa na
namna ambavyo WMO inaweza kusaidia katika maeneo mbalimbali yahusuyo hali ya
hewa ikiwa pamoja na mafunzo na vifaa vya hali ya hewa. Aidha aliipongeza TMA
katika juhudi zake za utekelezaji wa programu za WMO na kuzisaidia nchi zingine
za Afrika. Aliongeza kwa kusema kuwa TMA ni taasisi ya mfano Afrika katika
utoaji wa huduma bora za hali ya hewa
Nae mkurugenzi mkuu
wa TMA dkt. Agnes Kijazi aliwashukuru
Prof. Taalas kwa uamuzi wake wakutembelea Tanzania na alimuahidi kuwa Tanzania
kupitia TMA itaendelea kutekeleza makubaliano yote ya kimataifa yahusuo huduma
za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa program za WMO
Ikumbukwe
kuwa WMO huratibu na kusaidia katika kuboresha huduma za hali ya hewa katika
nchi kama vile kuanzisha mitandao ya ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuweka
miongozo inayosaidia utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa viwango na ubora wa
kimataifa n.k
Kupitia
WMO Tanzania na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imenufaika na kuongezewa uwezo
kupitia mafunzo, miundombinu ya hali ya hewa, hushiriki kikamilifu katika
shughuli za jopo la sayansi la kimataifa la ufuatiliaji wa mabadiliko ya hali
ya hewa (Intergovernmental Pannel on Climate Change - IPCC). Pia, kushiriki
katika shughuli za kongamano la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya
mabadiliko ya tabia nchi hasa masuala ya kisera (United Nations Framework for
Climate Change Conference - UNFCCC) ambapo mabadiliko ya hali ya hewa
yanayotokea Tanzania hujumuishwa katika makubaliano ya kimataifa kwa ajili ya
utekelezaji kimataifa na kitaifa kwa faida ya nchi yetu.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA
UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
PICHA
1. Katibu Mkuu wa WMO Prof
Petteri Taalas katika picha ya pamoja na menejimenti ya TMA
2. Katibu Mkuu wa WMO
Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa kutoka
TMA Bw. Chuki Sangalugembe kuhusiana na mtambo mkubwa wa kompyuta (Computer
Cluster) namna unavyosaidia katika uandaaji wa taarifa za hali ya hewa.
3. Katibu Mkuu wa WMO
Prof Petteri Taalas akichangia jambo baada ya kupata maelezo ya mfumo wa kisasa
utoaji taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa anga wakati alipotemebelea ofisi
za hali ya hewa zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Julius
Nyerere. hewa.
4. Katibu Mkuu wa WMO
Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa meneja wa kituo kikuu cha
utabiri Bw. Samuel Mbuya namna ya kuandaa utabiri wa hali ya hewa
5. Katibu Mkuu wa WMO
Prof Petteri Taalas akishuhudia na kushiriki mkutano wa kuandaa utabiri wa siku
unaofuatilia hali mbaya ya hewa kwa nchi za Afrika mashariki zilizoko katika
Bonde la Ziwa Victoria.
6. Katibu Mkuu wa WMO
Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa meneja wa mtandao wa vituo vya
hali ya hewa nchini Bi. Hellen Msemo kuhusiana na studio ya TMA inayohusika
katika kurekodi utabiri wa hali ya hewa wa kila siku.
7. Katibu Mkuu wa WMO
Prof Petteri Taalas akipata maelezo ya namna ya kuwaandikisha wakulima katika
mfumo wa utoajia taarifa za hali ya hewa kilimo kupitia simu za mkononi uitwao
FARMSMS kutoka kwa meneja wa huduma za matumizi ya taarifa za hali ya hewa Bw,
Isack Yonah

No comments:
Post a Comment