![]() |
| Tetemeko hili lilisababisha watu kuchanganyikiwa |
Maafisa
wa idara ya kudhibiti majanga wanasema mamia ya watu wamejeruhiwa vibaya kwa
tukio hilo lililotokea Jumapili. Tetemeko hilo lenye nguvu ya 7 kwenye vipimo
vya Richter limeharibu vibaya miundombinu ya umeme na barabara sambamba na
nyumba.
Katika kisiwa jirani
cha Bali picha za video zimeonyesha watu wakikimbia majumbani mwao huku
wakipiga kelele za msaada.Tetemeko hili limekuja wiki moja baada ya jingingine
kuipiga sehemu hiyo ya Lombok, kisiwa maarufu kwa shughuli za utalii ambapo
watu 16 waliuawa.
Hatari ya kuwepo kwa
kwa kimbunga ilitangazwa kisiwani hapo lakini ikaondolewa saa chache baadae. Msemaji
wa idara ya kudhibiti majanga ya Indonesia amesema nyumba nyingi zimeathirika
vibaya, ambapo nyingi kati ya hizo zilijengwa kwa kutumia nyenzo duni.
Waziri wa mambo ya
ndani wa Singapore Kasiviswanathan Shanmugam alikua ziarani katika kisiwa hicho
ambapo ametuma picha kwenye mitandao ya kijamii akionyesha namna chumba chake
kilivyoathirika.
Mtu huyu ambaye
hakutaja jina lake anasema alikua katika shughuli zake wakati tetemeko hilo
likitokea.
''Wakati natembea
nilisikia mingurumo, taratibu, taratibu, aada ikawa mikubwa na watu wakaanza
kukimbia wakisema ''tetemeko'' kila mmoja wetu alichanganyikiwa na kutoka nje
ya nyumba, maafisa usalama wakasema kila mtu atoke ndani.''
Daktari Ketut
Sudartana, wa Hospitali ya Sanglah Mjini Bali anasema wameamua kuwatibia
wagonjwa nje ili kuhakikisha usalama wao.
''Kwa wakati huu
tutawatibua wagonjwa hapa nje, na kwenye sehemu ya wazi ya mazoezi. Tutaweka
mahema ya dharura nje kwa msaada a BPBP ili kuwahihadhi wagonjwa wote pale, ili
madaktari na manesi wetu waweze kuwahudumia vizuri zaidi.''
Rais wa Indonesia Joko Widodo amesema serikali
yake inafanya jitihada za kutosha kunusuru maisha ya majeruhi huku akituma
salam za rambirambi kwa familia za wafiwa.
-BBC


No comments:
Post a Comment