![]() |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati)
akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya kilosa mara baada
ya kumaliza kufanya mkutano wa
Menejimenti ya Hifadhi ya taifa ya Mikumi uliofanyika jana katika ofisi za
Hifadhi hiyo wilayani Kilosa mkoani
Morogoro. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi.
![]() |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati)
akizungumza jambo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Ole Meng’ataki
(kushoto) mara baada ya kumaliza kufanya mkutano wa Menejimenti ya Hifadhi ya
taifa ya Mikumi uliofanyika jana katika ofisi za Hifadhi hiyo wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi.
![]() |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kushoto)
akizungumza na baadhi ya watalii wa ndani aliokutana nao jana wakati
alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa ajili ya kuzungumza na Menejimenti
ya Hifadhi hiyo.
![]() |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na
Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya
Mikumi wakati alipowatembelea jana katika ofisi za Hifadhi hiyo wilayani Kilosa mkoani Morogoro. (PICHA
ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
NA LUSUNGU
HELELA-MOROGORO
SERIKALI imesema
inaandaa kanuni zitakazoruhusu kufanyika uwindaji wa kiasili (Local
Hunting) kwenye maeneo ya wazi kwa ajili ya kitoweo ili wananchi waweze
kunufaika moja kwa moja na Maliasili zao ili waone umuhimu wa kuhifadhi.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema hayo jana wakati alipokuwa
akizungumza na Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiwa ni muendelezo wa
ziara zake za kikazi mkoani Morogoro kwa ajili ya kutatua changamoto
mbalimbali zinazoikabili Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
Amesema wawindaji hao
watapewa vibali maalum vitakavyowawezesha kuwinda kwa ajili ya kujipatia
vitoweo vya nyamapori na kutakuwa na maeneo maalum kwa ajili ya kuuzia
vitoweo hivyo kwa jamii.
Aidha, Ametaja aina za
vitoweo vitakavyokuwa vinauzwa kwenye maeneo hayo maalum ikiwa
pamoja na nyama ya mamba, nyati,swala viboko na wengineo.
Kwa upande wake,
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi za Taifa za Mikumi, Godwell Ole Meng'ataki amesema
kama kutakuwa na utaratibu mzuri itaweza kusaidia kuongeza mapato kwa nchi.
Aliongeza kuwa
utaratibu huo wa kuwa na sehemu maalum ya kuuzia vitoweo si mgeni kwa vile nchi
kama Afrika Kusini wamekuwa wakifanya hivyo na pia wana maeneo maalum kwa ajili
ya kuuzia viteweo vya nyamapori.





No comments:
Post a Comment