NMB YATOA MAFUNZO KWA ZAIDI YA VYAMA VYA MSINGI 1, 000 VYA USHIRIKA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 11 August 2018

NMB YATOA MAFUNZO KWA ZAIDI YA VYAMA VYA MSINGI 1, 000 VYA USHIRIKA

Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania - Benjamin Mkapa akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa NMB Bank – Ineke Bussemaker ikiwa ni shukrani kwa udhamini wa Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika atika viwanja vya Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu. NMB ilikuwa mmoja wa wadhamini wakuu wa maonesho hayo. 

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,Jenesta Mhagama(kulia) akiwakabidhi Meneja Uhusiano Biashara za serikali wa benki ya NMB,Christabel Hiza(kushoto) na Meneja Uhusiano Mwandamizi idara ya Kilimo biashara,Oscar Rwechungura kombe la ushindi wa kwanza taasisi za fedha kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo Kanda ya Kaskazini Nanenane Themi mkoa wa Arusha.

Sehemu ya madhimiso  ya kilele cha Siku ya Wakulima nchini (Nane nane).


Na Mwandishi Wetu, SIMIYU

BENKI ya NMB imetoa mafunzo kwa zaidi ya Vyama Vya Msingi 1, 000 vya Ushirika wa
Wakulima (AMCOS) ya kilimo na utunzaji fedha ndani ya Mwaka mmoja yenye lengo la
kuboresha sekta ya kilimo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika madhimiso ya kilele cha siku ya
wakulima nchini (Nane nane) Mkoani Simiyu, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB -
Ineke Bussemaker alisema benki yake imemaua kusaidia kuboresha sekta ya kilio
kutokana na umuhimu wake katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na pia
kuboresha uchumi wa wakulima.

Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo bado yanaendelea sehemu mbali mbaloi nchini
yanatariwa kuwafikia wakulima wengi zaidi kupitia vyama vya ushirika na hivyo
vitawezesha kuboresha kilimo na kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika ngazi ya jamii na
nchi kwa ujumla.

Alisema kuwa sekta ya kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi na kuajiri watanzania
zaidi ya asilimia 70, hivyo inapaswa kuboreshwa ili kutoa mchangomkubwa katika
maendeleo ya kiuchumi.

Bi. Bussemaker alisisitiza kuwa unatakiwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa
mendeleo ili kusaidia sekta ya kilimo kukua kwa haraka na kuleta tija kwa wakulima na
nchi kwa ujumla na kuwa ikiachiwa serikali peke yake haitaweza kuleta mabadiriko hayo
kwa haraka.
Alisema kuwa benki yake inaamini kuwa sekta ya kilimo inao uwezo mkubwa wa kuleta
mapinduzi ya kweli katika uchumi endapo kilimo kitaboreshwa nchini na kwamba sekta
hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa
viwanda.

Bi. Bussemaker alisema kuwa mbali na mafunzo hayo benki yake imekwisha tumia zaidi
ya shilingi bilioni 100 katika kuboresha sekta ya kilimo nchini kwa kutoa mikopo
mbalimbali pamoja na huduma zingine za kifedha kwa wakulima nchini.

“Ndani ya miaka michache ijayo, tunatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 500 katika
sekta kuwezesha shughuli za kilimo katika mnyororo mzima wa thamani, hivyo
nawaomba wakulima kuto kukata tamaa na kilimo kwani benki yao ipo pamoja nao
katika kuhakikisha inaleta mageuzi ya kilimo kwa manufaa na amendeleo ya wakulima
na nchi kwa ujumla” alisema Bi. Bussemaker.

Bi. Bussemaker aliwataka wakulima kutumia NMB Bank katika kuleta mageuzi chanya
katika kilimo na kuinua uchumi wa Tanzania kufikia uchumi wa kati kwa kuzalisha
malighafi zaidi ndani ya nchi ambazo zitatumika katika viwanda vilivyopo nchini kwa
kuwa mkulima akilima zaidi viwanda vinapata malighafi zaidi.

No comments:

Post a Comment