Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke
Bussemaker akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa bidhaa mpya za
benki hiyo, ikiwemo na ile ya mteja kwa simu yake kujifungulia akaunti popote
alipo.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
(BOT), Benard Kibesse (kushoto) na mgeni rasmi katika uzinduzi wa bidhaa mpya
za NMB, akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa bidhaa hiyo ya NMB
leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa
wakishuhudia hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Benki ya NMB leo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakijaribu
huduma za NMB kwa kutumia simu zao.
| Baadhi ya wageni waalikwa wakishuhudia hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam. |
BENKI ya NMB sasa imeendelea
kuboresha huduma za kibenki nchini hasa kuvutia kila raia kumiliki akaunti ya
benki kwa matumizi mbalimbali katika shughuli za kila siku. Ili kuhakikisha suala
hilo linatekelezeka, NMB imekuja na huduma iliyoboreshwa zaidi nay a kisasa
ambapo kila Mtanzania anaweza kujifungulia akaunti yake kupitia simu yake ya
mkononi aina yoyote ile.
Akizinduwa huduma hiyo leo jijini Dar
es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Benard Kibesse ameipongeza
Benki ya NMB kwa kuwa wabunifu wa kutumia teknolojia ambayo inachochea wananchi
kutolazimika kutembea na fedha wakati wote kwenye mahitaji yao.
Alisema utaratibu wa watu kutembea na
fedha mfukoni kwa ajili ya matumizi unapitwa na wakati na nihatari kwa usalama
wa mtu na fedha zake hivyo kuna kila sababu ya kuja na suluhisho kama la NMB.
Awali akifafanua juu ya huduma hizo,
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema kwa sasa bila kujali
aina ya simu anayotumia Mtanzania, anaweza kujifungulia akaunti yake akiwa
nyumbani au popote pale kwa kutumia simu yake.
Alisema huduma ya kujifungulia
akaunti hiyo ni rahisi na inaweza kukamilika ndani ya dakika tatu kisha unapata
akaunti yako huku namba yako ya simu ikiwa ndio namba ya akaunti hiyo. Alisema
huduma hiyo inaweza pia kufanyika kwa kutumia NMB Klik App kwa wenye simu janja
(smart phone).
Alisema NMB inakuwa ni benki ya
kwanza kutoa huduma ya mteja kujifungulia akaunti yake pasipo kutembelea tawi
la benki au kuitaji mlolongo wa makaratasi. Anasema mara baada ya kuwa na
akaunti hiyo mteja anaweza kuanza kuitumia papo hapo kwa shughuli zote za
kibenki bila makato ya kila mwezi.
“…Lengo la NMB ni kumfikia kila
Mtanzania na kumpa huduma za kibenki ili kumuingia katika mfumo rasmi wa
kiuchumi na maendeleo. Kuingia kwenye huduma hii mteja anatakiwa kupiga
*150*66# au ku-pakuwa NMB Klik App (Google Play au App Store) kwa wateja wa
simu janja kisha kuanza kujihudumia…,” alisema Bi. Bussemaker katika uzinduzi
huo.
Aliongeza ndani ya huduma hizo mteja
anaweza kufanya huduma mbalimbali kwa kutumia simu na NMB Klik App kama vile,
kupata mkopo, kulima bili anuai, kufanya malipo ya manunuzi mbalimbali nje na
ndani, kuwekeza fedha na kupata faida, malipo ya fedha za kigeni na hata
kufanya mahesabu na miamala ya kifedha.

No comments:
Post a Comment