MATUKIO PICHA TUKIO LA MAZISHI YA DADA MONICA MAGUFULI MKOANI GEITA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 22 August 2018

MATUKIO PICHA TUKIO LA MAZISHI YA DADA MONICA MAGUFULI MKOANI GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa  Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsaidia  Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakuweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Monica Joseph Magufuli likipelekwa Kanisani kwa ajili ya Misa takatifu Chato Mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kanisani katika Misa takatifu ya kumuombea Marehemu Dada yake Monica Magufuli. Wengine katika picha ni Mama yake Suzana Magufuli, Stanslaus Lori Madulu(Mme wa marehemu) , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na viongozi mbalimbali wa Kiserikali. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkewe Mama Marry Majaliwa wakitoa heshma zao za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Baba Askofu mkuu Mwandamizi  Yuda Thaddeus Ruwaichi akiongoza Misa ya kumuombea Marehemu Monica Magufuli Chato mkoani Geita

No comments:

Post a Comment