RAIS DKT. SAMIA AMUAPISHA DKT. MWIGULU NCHEMBA KUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA, IKULU DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Friday, 14 November 2025

RAIS DKT. SAMIA AMUAPISHA DKT. MWIGULU NCHEMBA KUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA, IKULU DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba miongozo ya utendaji kazi mara baada ya kumuapisha kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa kuimarisha kasi ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa ili kutimiza kwa wakati malengo ya kitaifa. Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya kumuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.) kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika Ikulu Chamwino. 
Katika hotuba yake, Rais Dkt. Samia amempongeza Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, akibainisha kuwa uteuzi wake umefanyika kufuatia tathmini ya kina ya sifa na uwezo alionao, hususan ufanisi wake katika kuwahudumia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Vilevile, amemtaka Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo zilizopo na kuongeza kasi ya utekelezaji na ufuatiliaji wa karibu wa shughuli za Serikali ili malengo ya Serikali yatimie kwa muda uliopangwa. 
Halikadhalika, Rais Dkt. Samia amemtaka Waziri Mkuu kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya nchi na bila upendeleo. Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia ametambua na kupongeza kazi kubwa iliyofanywa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, na amemshukuru kwa utumishi wake uliotukuka na kumtakia heri katika majukumu yake yajayo.

No comments:

Post a Comment