RAIS DKT. SAMIA AMTEUWA MWIGULU NCHEMBA KUWA WAZIRI MKUU MPYA... - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 13 November 2025

RAIS DKT. SAMIA AMTEUWA MWIGULU NCHEMBA KUWA WAZIRI MKUU MPYA...

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteuwa Bw. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu kuwa Waziri Mkuu mteule ambaye Bunge la Tanzania, linatakiwa kuthibitisha jina lake kwa kupigiwa kura.

Jina la Bw. Mwigulu Lameck Nchemba (aliye kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Serikali iliyopita) limewasilishwa muda huu bungeni na mpambe wa Rais, kwa ajili ya uthibitisho kwa kupigiwa kura. Bw. Nchemba ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa CCM ambaye amekuwa Waziri wa Fedha na Mipango tangu 31 Machi 2021.

Historia fupi ya Waziri Mkuu huyo mteule, alisomea uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam alipohitimu shahada ya uzamili kwenye mwaka 2006.

Alichaguliwa kuwa mbunge wa Iramba Magharibi mwaka 2010 akarudishwa bungeni kwa miaka 2015 – 2020. Mwaka 2015 alikuwa Naibu Waziri ya Fedha. Baada ya uchaguzi wa 2015 aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, ila mwaka 2016 alibadilishwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani, kabla tena ya kurejea nafasi ya Waziri wa Fedha.

No comments:

Post a Comment