DKT. MWIGULU AKAGUA MIUNDOMBINU NA MALI ZILIZOHARIBIWA NA VURUGU ZA OKTOBA 29, 2025 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 24 November 2025

DKT. MWIGULU AKAGUA MIUNDOMBINU NA MALI ZILIZOHARIBIWA NA VURUGU ZA OKTOBA 29, 2025

 








WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 24, 2025 amekagua miundombinu ya usafiri wa mwendo kasi pamoja na mali nyingine ikiwemo nyingine zilivyoharibiwa kutokana na  vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 jijini Dar es Salaam.

Maeneo yaliyokaguliwa ni pamoja na Kituo cha Mafuta cha Puma ilichopo kimara baruti, vituo vya mwendo kasi vya Kimara Korogwe na Kimara Mwisho pamoja na kituo cha Mafuta cha Rupees kilochopo Kimara Stop Over.

Baadhi ya Miundombinu ya Umma na mali za watu binafsi zilizoharibiwa kutokana na vurugu za Oktoba 29, 2025.

Mheshimiwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 24, 2025 amekagua miundombinu hiyo na kuwakumbusha watanzania umuhimu wa kuitunza Tanzania.

Pia Dkt. Mwigulu amewataka Watanzania kuamka kwani wanaoshawishi kufanya vurugu hawaipendi Tanzania, “tuilinde pamoja na miundombinu yake”.

“Wanajipa haki kwamba wao wanaipenda Tanzania, mpenda Tanzania hawezi kukwambia uichome Tanzania, msiwasikilize, mkiichoma zaidi Tanzania wao ndio wanalipwa zaidi”- Alisisitiza Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu.







YALIYOJIRI WAKATI WA ZIARA YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amekagua miundombinu ya Umma pamoja na mali zilizoathiriwa na vurugu iliyotokea Oktoba 29, 2025.

▪Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza hakutakuwa na maadhimisho ya Sherehe za Uhuru Desemba 09 na badala yake fedha ambazo zilipaswa kutumika katika Sherehe hizo zitumike  katika kurekebisha Miundombinu iliyoharibika kutokana vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025.

▪Wapatieni kazi wakandarasi wazawa, wanauwezo, hata kazi wanazopewa wageni, wakandarasi wazawa ndio wanafanya hizi kazi.

▪Maeneo ambayo kazi inaweza kufanywa na mtanzania ifanywe na Mtanzania, hata maeneo ambayo biashara inaweza kufanya na mtanzania ifanywe na mtanzania, Tanzania ni ya Watanzania.

▪Mfanyakazi yoyote mzembe na mlarushwa msimhamishe, mfukuzeni kazi, vijana wakitanzania ambao wanafanya kazi vizuri wako wengi

▪Ninaungana na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa wote walioathirika na vurugu zilizotokea oktoba 29, 2025

▪Tumuunge mkono Rais na wajumbe wa tume iliyoundwa kwa ajili kuchunguza kwenye undani tukio la vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 ili tujue namna lilivyofanyika na hatua stahiki zitakazochukuliwa

▪Nimepitia na kukagua uharibifu wa mali na miundombinu ya umma, huwezi kuamini kama tukio hili limetokea Tanzania 

▪Watanzania tunapaswa kujua miundombinu hii ni mali ya umma, tunazijenga kwa fedha zetu sisi watanzania, si pesa za Serikali.

▪Wanaoshabikia uharibifu wa Miundombinu ya Umma hawapo hapa nchini, wanawaambia mkachome mali za umma, mkifanya hivi mtaishije? huko wanakoishi haya wanayowaambia mfanye huko kwao hauwezi kuyafanya.

▪Wanajipa haki kwamba wao wanaipenda Tanzania, mpenda Tanzania hawezi kukwambia uichome Tanzania, msiwasikilize, mkiichoma zaidi Tanzania wao ndio wanalipwa zaidi.

▪Nchi zote ambazo zinarasilimali nyingi ndizo zinasababishiwa Vurugu, Tanzania ni nchi yenye Rasilimali adhimu ikiwemo Gesi na madini, rasilimali hizi tutazilinda kwa nguvu zetu zote.

▪Watanzania amekeni hawa wanaotushawishi kufanya vurugu hawatupendi, nawaomba vijana wa Tanzania, Mungu ametupa nchi nzuri, tuilinde pamoja na miundombinu yake.

▪Viongozi wa dini kuweni makini ya namna wanavyotaka kuwagonganisha, kaeni kwenye vikao vyenu, tuifanye Tanzania yetu iwe pamoja

▪Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anadhamira ya dhati ya kuiona Tanzania inakuwa moja na kuendeleza umoja wa Watanzania.

▪Wizara ya Ujenzi, TANROADS, DART, UDART, OWM-TAMISEMI husisheni wadau wengine ili ndani ya siku 10 shughuli katika jiji la Dar es Salaam zirejee kama kawaida, wekeni mpango wa haraka wa kurejesha wakati tunasubiri mpango mkubwa, baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, Watanzania tuilinde miundombinu hii.

▪Wanaoshawishi tuchome moto vitu wanaturudisha Watanzania kwenye umasikini.

No comments:

Post a Comment