| Mhadhiri kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma(SJMC), Dk. Egbert Mkoko akiwasilisha mada yake kwa washiriki wa semina hiyo. |
| Mwenyekiti wa TBN, Bw. Beda Msimbe akizungumza katika semina hiyo. |
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewapa
semina wamiliki wa mitandao ya kijamii Tanzania (TBN) ili kuhakikisha
wanazingatia maadili na kanuni katika kuripoti habari za Uchaguzi Mkuu 2025
unaotarajia kufanyika Oktoba.
Mafunzo hayo yaliojumuisha Bloggers pia wa TBN kutoka baadhi ya mikoa walioshiriki kupitia mtandao wa ‘Zoom” yamefanyika leo jijini Dar es Salaam Ukumbi wa Mikutano wa TCRA.
Miongoni mwa maeneo yaliogusiwa katika mafunzo ni namna ya kuzingatia Sheria na Maadili kwa Wanahabari, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa vyama vya Siasa za Mwaka 2020 pamoja na kuzingatia Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika uandishi wa habari za uchaguzi.
Akiwasilisha mada ya Mwongozo wa Waandishi wa
Habari katika uandishi wa habari za uchaguzi, Mhadhiri kutoka Shule Kuu ya
Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), Dk. Egbert Mkoko aliwataka
wanahabari hao kuzingatia sharia na kanuni katika kazi zao ili kuepuka mkanganyiko.
Katika mafunzo hayo, Dk. Darius Mukiza wa SJMC
aliwasilisha mada ya Matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Akili Unde (AI)
kuelekea Uchaguzi Mkuu, huku Bi. Rehema Mpagama toka Bodi ya Ithibati ya
Wanahabari, akiwanoa wanahabari hao juu ya Maadili na Sheria kwa Waandishi wa
Habari.
Mada zingine zilizowasilishwa ni, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa vyama vya Siasa za Mwaka 2020, ikiwasilishwa na Mhandisi Andrew Kisaka toka TCRA na mada ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuelekea Uchaguzi Mkuu ikiwasilishwa na Bw. Innocent Mungy – Mkuu wa Mawasiliano Serikalini Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC).
| Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, ambao ni waandaaji wa mafunzo hayo, Mhandisi Andrew Kisaka akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo, |
Awali akizungumza katika semina hiyo, Mwenyekiti wa TBN, Beda
Msimbe ameishukuru TCRA kwa ushirikiano wanaoutoa kwani kitendo hiki
kinaendelea kuwajenga kundi hili la wanahabari katika uandaaji wa maudhui yao
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

No comments:
Post a Comment