
Meneja Uendeshaji wa Maabara ya ALIRA, Bw. Maliki Alan akitoa elimu kwa umma kuhusu maabara hiyo inavyofanya kazi.
Na Dunstan Mhilu
MENEJA Mwendeshaji wa ALIRA Dental Labaratory iliyopo Mtaa wa Mazengo Upanga Dar es Salaam, Maliki Alan amesema huduma ya Kinywa na meno nchini imeimarika maradufu ikilinganishwa na hapo awali ambapo huduma hiyo kwa umadhubuti zaidi ilikuwa ikifanyika nje yanchi.
Maliki ameyasema hayo katika mahojiano na chombo hiki kwenye kongamano la siku mbili linalohusu masuala ya Kinywa na meno yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na zaidi ya mataifa kumi ikiwemo China, Marekani, Uganda, Kenya na Namibia.
“Niukweli usiopingika Ndugu Mwandishi nchi yetu imepiga hatua kubwa katika uwekezaji wa sekta ya afya ikiwemo idara ya kinywa na meno nah ii nikutokana na kukubali kufanya kazi na sekta binafsi ikiwemo ALIRA,” Amesema Maliki.
Maliki aliongeza kwamba Maabara yao hufanya matengenezo ya meno bandia na hutibu kinywa kwa ujumla na mgonjwa kurejea katika hali yake ya kawaida na kwa mtu ambaye hujui kwamba alikuwa ni kibogoyo huwezi jua kabisa kwani hana tofauti na binadamu mwingine.
“Huduma zetu zipo hapa Dar es Salaam na hupatikana mikoani kote na tunatoa huduma pia kwa mataifa mbalimbali, na kama kuna kitu tunajivunia nikuwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anayekubali kushirikiana na wafanyabiashara binafsa na sisi tunaunga mkono jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo hususani kuimarisha huduma ya afya,” amesema Maliki.
Awali akizungumza wakati wa hafla ya kongamano hilo la kimataifa la wadau wa afya ya kinywa na meno Balozi John Ulanga amesema nchi kama nchi imepiga hatua kubwa sana na hivyo serikali ya awamu ya Sita inahitaji maua yake.
“Matunda hayo mnayoyaona leo ni jitihada madhubuti za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha anashirikiana na sekta binafsi kuwaletea wananchi maendeleo kwakuweka mazingira wezeshi,” amesema Ulanga.
Aidha Maliki alihitimisha kwakusema kwamba Maabara yao inatumia teknolojia ya kisasa kutoka nchini ujerumani na huuza pia vifaa tiba serikalini na vituo vya afya binafsi.

No comments:
Post a Comment