Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kida amesema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kujadili namna kuhuisha mbinu za mashauriano na sekta binafsi na kupata mapendekezo yanayohusu changamoto za Kodi na sizizo za kikodi ili kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na mazingira Bora ya Biashara na Uwekezaji na Mifumo imara ya kikodi.
Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mheshimiwa Balozi Ombeni Sefue na Wajumbe wa Tume hiyo, na Mwenyekiti wa Wataalamu wa MKUMBI II, Prof. Faustine Kamuzora.


No comments:
Post a Comment