|
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB,
Filbert Mponzi (kushoto) akimkabidhi moja ya mavazi ya wakandarasi kazini Naibu
Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya mara baada ya kuzinduwa rasmi Maboresho
ya Huduma za Kibenki kwa Makandarasi Wazawa. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Bodi ya Usajili wa
Makandarasi (CRB), Eng. Ally Mwita akishuhudia. |
|
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB,
Filbert Mponzi (kushoto) akimkabidhi Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey
Kasekenya vifaa vya ujenzi mara baada ya kuzinduwa Maboresho ya Huduma za Kibenki kwa Makandarasi
Wazawa, ambapo imeongeza Kiwango cha Dhamana za Kuombea Kazi kutoka Sh. Bilioni
2.5 hadi Sh. Bilioni 5, kiwango cha Dhamana za Miradi kutoka Sh. Bilioni 1.5 hadi
Sh. Bilioni 3. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Bodi ya Usajili wa
Makandarasi (CRB), Eng. Ally Mwita. |

Filbert Mponzi akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maboresho ya Huduma za
Kibenki kwa Makandarasi Wazawa, ambapo imeongeza Kiwango cha Dhamana za Kuombea
Kazi kutoka Sh. Bilioni 2.5 hadi Sh. Bilioni 5, kiwango cha Dhamana za Miradi
kutoka Sh. Bilioni 1.5 hadi Sh. Bilioni 3. |
|
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya akizungumza kwenye hafla
ya uzinduzi wa Maboresho ya Huduma za Kibenki kwa Makandarasi Wazawa, ambapo imeongeza
Kiwango cha Dhamana za Kuombea Kazi kutoka Sh. Bilioni 2.5 hadi Sh. Bilioni 5, kiwango
cha Dhamana za Miradi kutoka Sh. Bilioni 1.5 hadi Sh. Bilioni 3 |
|
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo kwenye hafla
ya uzinduzi wa Maboresho ya Huduma za Kibenki kwa Makandarasi Wazawa, ambapo imeongeza
Kiwango cha Dhamana za Kuombea Kazi kutoka Sh. Bilioni 2.5 hadi Sh. Bilioni 5, kiwango
cha Dhamana za Miradi kutoka Sh. Bilioni 1.5 hadi Sh. Bilioni 3 |
|
Baadhi ya washiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Maboresho
ya Huduma za Kibenki kwa Makandarasi Wazawa, ambapo imeongeza Kiwango cha
Dhamana za Kuombea Kazi kutoka Sh. Bilioni 2.5 hadi Sh. Bilioni 5, kiwango cha
Dhamana za Miradi kutoka Sh. Bilioni 1.5 hadi Sh. Bilioni 3. |
|
Picha ya pamoja meza kuu kwenye hafla hiyo. |
NAIBU Waziri wa Ujenzi Eng.
Godfrey Kasekenya amewataka Wakandarasi nchini kutumia vizuri fursa za kibenki
kukuza mitaji na hivyo kumudu kupata miradi mikubwa ya ujenzi ili kukuza uchumi
binafsi na taifa kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Kasekenya
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa
Maboresho ya Huduma za Kibenki kwa Makandarasi Wazawa, kwa Benki ya NMB ambapo imeongeza
Kiwango cha Dhamana za Kuombea Kazi kutoka Sh. Bilioni 2.5 hadi Sh. Bilioni 5, kiwango
cha Dhamana za Miradi kutoka Sh. Bilioni 1.5 hadi Sh. Bilioni 3.
Akifafanua zaidi, Naibu Waziri
Kasekenya amesema fursa hizo zinaendana na mikakati ya Serikali ya kukuza
uchumi wa wakandarasi wazawa na hivyo kusababisha fedha nyingi za miradi ya
ujenzi kubaki nchini badala ya kwenda nje ya nchi.
"Uaminifu, weledi na
uzalendo kwa wakandarasi kutawezesha benki nyingi kutoa mikopo na fursa nyingi
na kukuza sekta ya wakandarasi", amesisitiza Eng. Kasekenya.
Aidha ameipongeza Benki ya
NMB kwa mikakati yake ya kuwawezesha Wakandarasi hususan wazawa hali itakayokuza sekta ya ujenzi nchini.
"Serikali inatarajia
fursa hizi na nyingine zitakazotolewa zitawawezesha wakandarasi wazawa
kushindana na wakandarasi wa nje na kupata miradi mikubwa ya ujenzi na hivyo
kuongeza ujuzi katika ujenzi wa miradi na kutoa fursa nyingi za ajira",
amesisitiza.
No comments:
Post a Comment