HUDUMA NA ELIMU YA AFYA MAONESHO YA NANENANE DODOMA ZALETA FARAJA KWA WANANCHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 7 August 2024

HUDUMA NA ELIMU YA AFYA MAONESHO YA NANENANE DODOMA ZALETA FARAJA KWA WANANCHI



Na Elimu ya Afya kwa Umma

WANANCHI kutoka maeneo mbalimbali wanaotembelea banda la Wizara ya Afya katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Kitaifa (Nanenane) Mkoani Dodoma, wamevutiwa na huduma zinazotolewa katika banda hilo.

Wakizungumza Agosti 7, 2024 baada ya kutembelea banda la Wizara ya Afya kwenye maonesho ya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma baadhi ya Wananchi hao akiwemo Jumanne Omary, Majaliwa Justine pamoja Bi.Yasinta Masaka wamesema wamesema huduma za Afya zinazotolewa katika banda la Wizara ya Afya zinavutia huku wakitoa wito kwa watu wengine kutumia fursa ya maonesho ya nanenane kupatahuduma za afya bila malipo.

"Huduma zao za afya ni nzuri sana hivyo nitoe wito kwa Wananchi wengine watumie fursa hii ," amesema Jumanne Omary kutoka Homanyika Dodoma.

"Nimepima afya ya macho na kupewa ushauri mzuri na Watalaamu wa Afya tena kwa ukarimu mzuri mno niwasihi na wengine kuacha kulala nyumbani raha ya afya yako ni Banda la Wizara ya Afya"amesema Yasinta.

Ikumbukwe kuwa katika Banda la Wizara ya Afya huduma mbalimbali zinatolewa kuanzia Elimu ya Afya, Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa, Chanjo dhidi ya Homa ya ini, Uviko 19, pamoja na Chanjo dhidi ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya Kizazi kwa wanawake.

Katika dawati la elimu na uhamasishaji kuna  wataalam wa masuala ya Afya ya Akili, Lishe na Tiba Asili.

Kwenye dawati hili pia utapata elimu ya Ugonjwa wa Virusi vya UKIMWI pamoja na huduma za upimaji VVU, Elimu ya Ugonjwa wa Malaria pamoja na upimaji, Kifua Kikuu, na hapa tuna Maabara tembezi ambayo ina vifaa vya kisasa vya upimaji na wataalam wetu watakupima ewe mwananachi na kubaini endapo una maambukizi ya TB.

Huduma za uchunguzi wa awali wa Saratani ya Mlango wa Shingo ya Kizazi kwa wanawake, Saratani ya Matiti, Huduma za Uzazi wa Mpango njia zote zinapatikana.

Huduma hizi zote zinatolewa bureee! Hima kwako mwananchi kuchangamkia maonyesho haya uweze kupata huduma hizi muhimu za afya.

Zipo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya zikiwemo, Taasisi ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI, Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA, Hospitali ya Benjamin Mkapa BMH, Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba TMDA, pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF ambao pia wanatoa huduma katika maonyesho haya.

No comments:

Post a Comment