WAZIRI MAKAMBA AKAGUA UJENZI OFISI YA WIZARA MTUMBA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 12 December 2023

WAZIRI MAKAMBA AKAGUA UJENZI OFISI YA WIZARA MTUMBA

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Lengo la kutembelea mradi huo ni kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi na kufanya mazungumzo na wasimamizi wa mradi ili kupata taarifa ya maendeleo ya mradi pamoja na kutumia fursa hiyo kusisitiza ukamilishwaji wa mradi kwa wakati na viwango vinavyotarajiwa.

Akizungumza na Mkandarasi anayesimamia mradi huo, Mhe. Makamba amepongeza hatua iliyofikiwa na amemtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi ili maradi huo ukamilike na kukabidhiwa kwa wakati.


“Pamoja na kazi nzuri iliyofanyika katika ujenzi wa jengo hili, bado kazi iliyobaki ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili mradi ukabidhiwe na jengo lianze kutumika na hatimaye kuleta haueni ya tatizo la uhaba wa ofisi kwa watumishi wa Wizara” amesema Mhe. Makamba


Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Makamba aliambatana na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samuel Shelukindo, na Balozi Stephen Mbundi anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki na watendaji wengine wa Wizara.


Jengo hilo litakalogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 22.9 hadi kukamilika kwake lilianza kujengwa mwezi Januari 2022. Ujenzi huo unaogharamiwa na Serikali unalenga kuziwezesha Wizara na Taasisi za Serikali kuwa na majengo ya kudumu katika mji wa Serikali.


Mradi wa ujenzi wa jengo hilo unatekezwa na Umoja wa Kampuni za Sole Works na Mshauri Mwelekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi. 

Mbali na kutembelea jengo la Wizara, Mhe. Waziri Makamba ametembelea Ofisi za Wizara zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na watumishi mbalimbali waliokuwa wakiendelea na utekelezaji wa majukumu yao katika ofisi hizo.

No comments:

Post a Comment