 |
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi ya
Shilingi Bilioni mbili kutoka kwa Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu kwa
ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika Mji mdogo wa Katesh,
Hanang Mkoani Manyara hivi karibuni. Hundi hiyo ni michango iliyochangwa na Taasisi
mbalimbali za Serikali na kuwasilishwa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10
Desemba, 2023. |
 |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip
Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya hafla fupi ya kupokea Hundi ya
michango kutoka Taasisi mbalimbali kwa ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea Katesh,
Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 10
Desemba, 2023. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip
Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses
Kusiluka, Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu pamoja na Wakuu wa Taasisi
mbalimbali za Serikali, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba,
2023.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais
Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani
Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.
 |
Viongozi mbalimbali
wakiwa kwenye hafla fupi ya upokeaji Hundi ya
michango kutoka Taasisi mbalimbali kwa
ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea
Katesh, Ikulu Mkoani
Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023. |
No comments:
Post a Comment