GPE NA CAMFED WAKUTANA NA ASASI ZA KIRAIA ZINAZOSHUGHULIKIA ELIMU NCHINI - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 29 November 2023

GPE NA CAMFED WAKUTANA NA ASASI ZA KIRAIA ZINAZOSHUGHULIKIA ELIMU NCHINI

 

Wawakilishi wa Asasi za Kiraia zinazojihusisha na maswala ya elimu wakichangia wakati wa mazungumzo hayo katika ofisi za CAMFED jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mkrugenzi wa Programu na Ushirikiano wa Taasisi  ya Campaign for Female Education (CAMFED) tawi la Tanzania Bi. Anna Sawaki alipowasili kuzungumza   na wawakilishi wa Asasi za Kiraia zinazojihusisha na maswala ya elimu katika ofisi za CAMFED jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi  ya Campaign for Female Education (CAMFED) tawi la Tanzania Bi. Nasikiwa Duke alipowasili kuzungumza   na wawakilishi wa Asasi za  Kiraia zinazojihusisha na maswala ya elimu katika ofisi za CAMFED jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wamekutana na kuzungumza   na wawakilishi wa Asasi za  Kiraia zinazojihusisha na maswala ya elimu katika ofisi za Taasisi  ya Campaign for Female Education (CAMFED) tawi la Tanzania jijini Dar es Salaam leo.


Mkurugenzi wa CAMFED Tanzania, Bibi Nasikiwa Duke, ameeleza kuwa lengo kuu la mazungumzo hayo ilikuwa ni kutoa msisitizo wa umuhimu wa kuipa kipaumbele sekta ya elimu katika ajenda za kijamii na  kisiasa.


Akiuongea baada ya kikao hicho Bi. Duke alisema mazungumzo hayo yalizingatia pia majukumu muhimu ya Asasi za  Kiraia katika kusaidia juhudi za serikali kuboresha sekta ya elimu na kuchangia kikamilifu kwenye mijadala ya kisera katika makundi ya elimu ya ndani na wadau wa sekta hiyo.


"Mazungumzo hayo yalitoa fursa kwa wawakilishi wa Asasi hizo za Kiraia kushirikiana na kubadilishana uzoefu wao Pamoja na mafanikio yo katika kusaidia maendeleo na mabadiliko ya mfumo wa elimu.


Kikao hicho  kiliwaleta pamoja wadau muhimu ili kuzungumzia umuhimu wa juhudi za  pamoja kuisaidia juhudi za serikali katika  kukuza elimu, haswa katika mikoa inayokabiliana na mahitaji makubwa zaidi," Bi Duke alifafanua.


GPE ni mfuko mkubwa zaidi wa duniani uliojitolea kusaidia maswala ya maendeleo ya utoaji wa elimu bora katika nchi zenye kipato cha chini na kuhakikisha kwamba kila mtoto, bila kujali jinsia, anapata fursa, matumaini na uwezo wa kusoma.


Katika miongo miwili iliyopita, GPE imekuwa ikitoa fedha na misaada kukuza mfumo wa elimu imara na thabiti katika nchi zilizoathiriwa na umaskini mkubwa au migogoro ili kuwezesha watoto  wengi zaidi, haswa wasichana, kupata elimu inayohitajika kwa ukuaji binafsi na kuchangia kujenga ulimwengu wenye ustawi  endelevu.


Kwa upande mwingine, CAMFED ni Taasisi iiliyojizatiti kushughulikia utoaji elimu kwa wasichana, kupitia mfumo wa uwajibikaji wa vijana na jamii unaoshajihisha matarajio ya wasichana kuwa wanawake huru na wenye ushawishi.


CAMFED inaendeshwa  na kamati na timu za mitaa zinazojumuisha wahitimu, walimu, wazazi, maafisa wa serikali, na wadau wengine wa kujitolea ambao hutenga muda na kutumia utaalam wao kuhakikisha kuwa wasichana wengi wanamaliza elimu yao kwa mafanikio.

No comments:

Post a Comment