BASHUNGWA AMKABIDHI MKANDARASI HENAN BARABARA KM 77.6 SINGIDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Saturday, 9 September 2023

BASHUNGWA AMKABIDHI MKANDARASI HENAN BARABARA KM 77.6 SINGIDA

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza kwenye hafla ya kumkabidhi mkandarasi Henan Highway Engineering Group Barabara ya Sabasaba - Sepuka - Ndago - Kizaga Km 77.6 ili ianze kujengwa kwa kiwango cha lami hafla iliyofanyika Misigiri Iramba mkoani Singida.

Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza kwenye hafla ya kumkabidhi mkandarasi Henan Highway Engineering Group Barabara ya Sabasaba - Sepuka - Ndago - Kizaga Km 77.6 ili ianze kujengwa kwa kiwango cha lami hafla iliyofanyika Misigiri Iramba mkoani Singida.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mhe. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba wakifurahia jambo kwenye hafla hiyo.

Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza kwenye hafla ya kumkabidhi mkandarasi Henan Highway Engineering Group Barabara ya Sabasaba - Sepuka - Ndago - Kizaga Km 77.6 ili ianze kujengwa kwa kiwango cha lami hafla iliyofanyika Misigiri Iramba mkoani Singida.

Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza kwenye hafla ya kumkabidhi mkandarasi Henan Highway Engineering Group Barabara ya Sabasaba - Sepuka - Ndago - Kizaga Km 77.6 ili ianze kujengwa kwa kiwango cha lami hafla iliyofanyika Misigiri Iramba mkoani Singida.

WAZIRI wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ameitaka Wakala wa Barabara nchini Tanzania (TANROADS) kumsimamia kikamilifu mkandarasi Henan Highway Engineering group anaejenga Barabara ya Sabasaba - Sepuka - Ndago - Kizaga Km 77.6 ili ikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Amesema hayo Misigiri Iramba mkoani Singida akizungumza katika hafla ya kumkabidhi mkandarasi ujenzi wa barabara hiyo.

"TANROADS jipangeni vizuri ujenzi ukamilike ndani ya muda uliokusudiwa na kwa ubora," amesema Mhe. Bashungwa. 

Waziri huyo wa Ujenzi amewataka wananchi watakaopata ajira katika mradi huo kuwa waaminifu, wabunifu na walinzi wa vifaa vya mkandarasi ili kutochelewesha mradi huo.

"Tunataka mradi huu uendane na thamani ya fedha iliyotolewa na tunaamini barabara hii itakapokamilika itachochea pia kukua kwa uchumi wa eneo hili, hivyo ni vema wananchi mkatumia fursa za biashara na uzalishaji wa mazao zitakazo jitokeza," Amesema Bashungwa. 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mohamed Besta amesema barabara hiyo inayounganisha wilaya za Singida, Ikungi na Iramba itahuisha uchumi kwa Mkoa wa Singida kwa kuwa inapita kwenye maeneo ya kilimo na madini.

Amesema zaidi ya shilingi bilioni 88.5 zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mradi huo.

Mbunge wa Iramba ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Mhe. Mwigulu Nchemba ameishukuru Serikali kwa namna inavyozifungua barabara za Mkoa wa Singida na kuwataka wakazi wa mkoa huo kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo. 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amemhakikishia Waziri wa Ujenzi kuwa vifaa vya mkandarasi vitalindwa na atapata ushirikiano wa kutosha ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Kukabidhi barabara hiyo kwa mkandarasi kunafuatiwa kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wake Agosti 7 mwaka huu.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi.

No comments:

Post a Comment