DART KUJENGA CHUO CHA MAFUNZO YA MADEREVA WA BRT, KITATOA MAFUNZO PIA KWA MADEREVA KUTOKA NJE YA NCHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 17 May 2023

DART KUJENGA CHUO CHA MAFUNZO YA MADEREVA WA BRT, KITATOA MAFUNZO PIA KWA MADEREVA KUTOKA NJE YA NCHI

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dkt. Elephas Mollel akizungumza wakati akiwasilisha moja ya mada katika semina ya kuwajengea uelewa wa waandishi kuhusu mradi wa BRT na shughuli mbalimbali za uendeshaji wa mradi huo, Semina hiyo inafanyika kwa siku tano kwenye hoteli ya Dodoma City jijini Dodoma.

Hellen Nachilongo Mwandishi wa habarikutoka gazeti la Citizen akiwasilisha majumuisho ya mada za siku ya jana katika semina hiyo inayoendelea kwenye hoteli ya Dodoma City jijini Dodoma.

Waandisi wa habari wakifuatilia mada kuhusu sheria iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dkt. Elephas Mollel katika semina hiyo.

NA JOHN BUKUKU, DODOMA

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) wanatarajia kujenga Chuo cha kutoa mafunzo kwa madereva ya mabasi yaendayo haraka jambo ambalo litasaidia kupunguza ajali ambazo zinazotokana na baadhi ya madereva kutokuwa makini pamoja na kukosa elimu namna bora ya kusimamia na kuendesha magari ya BRT.

Chuo cha BRT kinatarajiwa kujengwa Manispaa ya Kigamboni ambapo kitakuwa kinatoa mafunzo kwa ajili ya kuwafundisha madereva wa BRT pamoja na wengine wanaotoka ndani na nje ya Nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dodoma katika semina Maalam ya kuwajengea uwezo, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dkt. Elephas Mollel, amesema kuwa Chuo cha BRT kitakuwa na walimu pia kutoka nje ya nchi ambao wana uzoefu mkubwa wa kufundisha madera wa magari yaendayo haraka.

"Kutakuwa na walimu wenye uwezo mkubwa ambao watakuwa wanafundisha namna bora ya kuendesha na kusimamia mradi wa BRT" amesema

Ameeleza kuwa watakuwa wanatoka mafunzo kwa madereva kutoka Chuo BRT, lengo ni kutoa mafunzo baada ya chuo kujengwa na wataaza kuwafundisha madereva ambao tayari wameajiriwa na DART.

Amesema kuwa wanatambua uhiaji mkubwa wa miundombinu katika kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa wakati.

Dkt. Mollel amesema kwa sasa wapo katika utekelezaji miradi katika Mkoa wa Dar es Salaam, huku akibainisha kuwa awamu zote sita zikikamilika watakuwa wameajiri madereva zaidi ya 6,000 kutokana na magari yaendayo haraka 3,000 yatakayokuwepo kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri.

Hata hivyo amefafanua kuwa katika ujenzi wa maradi wa BRT Mbagala kuna dereva wa mwanamke ambaye amekuwa makini na hajawai kusababisha ajali.

"Ukiangalia ajali nyingi zinasababishwa na madereva wenyewe kwa kutokuwa makini, tunaomba wazazi wawapeleke vijana wao wa keki kusoma udereva ili waje kuendesha magari yaendayo haraka" amesema

Amesema kuwa kuna watoto wengi wa kike ambao wamemaliza shule wapo nyumbani ni vizuri wakijufunza masomo ya udereva kwani ni fani kama zilivyo nyengine.

No comments:

Post a Comment