WAZAZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA MAENDELEO YA MTOTO SHULENI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 23 April 2023

WAZAZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA MAENDELEO YA MTOTO SHULENI

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Juma la Elimu Kitaifa, ambaye pia ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi (kulia) akizungumza na wanajamii katika ziara za wadau wa elimu walipotembelea baadhi ya shule ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

 

Mheshimiwa Fatma Mwasa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (kushoto) pamoja na meza  kuu wakipata maelezo kutoka katika Banda la Uwezo Tanzania kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

Shamra shamra za Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Makame (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Juma la Elimu Kitaifa, ambaye pia ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.


Sehemu ya wazazi wakiwa katika moja ya mikutano ya ziara za wadau wa elimu walipotembelea baadhi ya shule katika Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

WAZAZI mkoani Morogoro na Tanzania kwa ujumla wametakiwa kubadilika na kuanza kuwa karibu zaidi na watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia masuala ya elimu ya watoto, ili kumjenga vizuri mtoto kwa kushirikiana na walimu.

Kauli hiyo, imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Juma la Elimu Kitaifa, ambaye pia ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi walipokuwa akizungumza kwenye mikutano ya uhamasishaji jamii juu ya ushiriki wa wazazi kuboresha maendeleo ya elimu katika maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa, Mvuha mkoani Morogoro.

Aidha alisema baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa ushirikiano baina ya wazazi na walimu unaboresha zaidi maendeleo ya elimu kwa watoto, jambo ambalo maeneo mengine kuna wazazi hujitoa katika ushirikiano hivyo kuathiri maendeleo ya elimu kwa watoto.

Aliongeza kuwa utafiti uliofanywa na Shirika la Uwezo Tanzania unaonesha ni asilimia 50 tu ya Wazazi ndio wanatembelea shuleni kuzungumza na walimu kuhusu maendeleo ya watoto wao, jambo ambalo linaitaji msukumo kwa wazazi kufanya mabadiliko ili kuboresha maendeleo ya elimu kwa watoto.

"Tunaamini kupitia shughuli za Maadhimisho ya Juma hili la Elimu mkoani Morogoro Jamii itabadilika na kuanza kuwa karibu na walimu ili kwa pamoja kuwasaidia watoto wapate elimu bora. 

Hata hivyo alisema pamoja na mambo mengine wazazi wanapaswa kutambua kuwa kuchangia chakula kwa watoto ni wajibu wao wala sio wajibu wa serikali, na uwepo wa mpango wa chakula shuleni pia huchangia watoto kufanya vizuri kwenye masomo yao.


Wanafunzi wakitoa burudani kwenye moja ya mikutano ya ziara za wadau wa elimu walipotembelea baadhi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment