RAS RUVUMA BINGWA MCHEZO WA BAO MICHEZO YA MEI MOSI 2023 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 25 April 2023

RAS RUVUMA BINGWA MCHEZO WA BAO MICHEZO YA MEI MOSI 2023

 

Bingwa mchezo wa bao kwa wanaume Bw. Emmanuel Komba kutoka RAS Ruvuma (kulia) akisoma mchezo wakati wa fainali ya mchezo huo dhidi ya mpinzani wake Hashimu Rashidi (kushoto) kutoka Mahakama Tanzania Aprili 25, 04, 2023 Morogoro.

Timu ya mchezo wa kamba ya Wizara ya Afya wanawake (kulia) wakiwavuta timu ya Mahakama Tanzania (kushoto) kwa mivuto 2-1 wakati wa nusu mchezo wa fainali wa kuvuta kamba kwa wanawake ambao umefanyika Aprili 25, 2023 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Timu ya mchezo wa kamba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanawake (kulia) wakiwavuta timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera (kuhoto) kwa mivuto 2-0 wakati wa nusu mchezo wa fainali wa kuvuta kamba kwa wanawake ambao umefanyika Aprili 25, 2023 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

TIMU ya RAS Ruvuma mchezo wa bao kwa wanaume imeibuka kidedea kwa kuwakilishwa vyema na Bw. Emmanuel Komba ambaye ni bingwa wa mchezo huo wakati mshindi wa pili ni Hashimu Rashidi kutoka Mahakama Tanzania na mshindi wa tatu ni Kassim Ambindwale kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

Kwa upande wa wanawake bingwa wa mchezo wa bao ni Martha Mwasumbi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, mshindi wa pili ni Ofrasia  Muhoha kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road na mshindi wa tatu ni Husna Omary kutoka Wakala wa Barabara. Tanzania (TANROADS).

Mchezo huo umefanyika Aprili 25, 2023 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro huku michezo ya mpira wa miguu, kamba wanawake na wanaume, mpira wa netiboli na mpira wa wavu wanawake na wanaume ikifikia hatua ya nusu fainali.

Timu zilizoingia hatua ya nusu fainali katika mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Afya wakati kwa upande wa wanaume timu zilizoingia hatua hiyo ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mahakama Tanzania, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) na Ofisi ya Rais Ikulu.

Kwa mchezo wa netiboli, timu nne ambazo zimeendelea kutembea kifua mbele kwa kukata tiketi ya hatua ya nusu fainali ni Ofisi ya Rais Ikulu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Katika mchezo wa mpira wa miguu, timu za Mahakama Tanzania wamewafunga Hazina 2-1 na kuungana na timu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambao wamewaadhibu Wizara ya Afya kwa kuwafunga 3-0 huku timu za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi watamenyana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao watapepetana na timu ya Mamlaka ya Maato Tanzania (TRA) kuungana na timu ambazo tayari zimekata tiketi ya hatua ya nusu fainali.

Kwa upande wa mpira wa wavu wanaume ambao wanacheza kwa mtindo wa ligi, timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wameifunga Morogoro DC kwa 2-1 na timu ya RAS Dodoma imewafunga timu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) 2-0 wakati kwa upande wa wanaume timu ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) imewafunga timu ya RAS Dodoma 2-0, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamewafunga Wizara ya Maliasili 2-0 na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wamewafunga timu ya RAS Morogoro 2-0.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Aprili 29, 2023 kwa mchezo wa fainali kwa michezo ya mpira wa miguu, mpira wa netiboli, mchezo wa kuvuta kamaba wanawake na wanaume pamoja na mchezo wa wavu wanawake na wanaume.


No comments:

Post a Comment