Thobias Mwanakatwe na Dotto Mwaibale, Singida
HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida imenunua
magari mawili ya kuzolea taka yaliyogharimu zaidi ya Sh.Milioni 200 ikiwa ni
mkakati wa manispaa hiyo kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya usafi.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jeshi Lupembe,
alisema magari hayo ambayo yatazinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter
Serukamba, yamenunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani zilizotengwa katika bajeti ya 2022/2023.
Alisema katika mapato hayo ya fedha za ndani
Manispaa inajenga kituo cha Afya Mtipa kwai Sh.milioni 500, kujenga machinjio
ya kisasa Sh.Milioni 120, kujenga jengo la utawala ghorofa tatu eneo la
karakana fedha kutoka serikali kuu Sh. bilioni moja kwa awamu ya kwanza na Sh.
milioni 31 zimetumika kulipa fidia ya dampo Mwankoko.
Lupembe amewaomba wananchi wa Manispaa ya Singida
kutoa ushirikiano kwa kuhifadhi taka taka kandokando ya barabara ili magari
hayo yatakapopita yaweze kuzichukua.
"Jukumu ya kuuweka mji katika hali ya usafi
ni la wananchi wote na sio la watendaji wa Manispaa, haipendezi kuona mtu anatupa
taka ovyo barabarani, sasa tumenunua haya magari tuyatumie ili kuuweka mji wetu
kwenye usafi," alisema Lupembe.
Aidha, Lupembe alihimiza wananchi kufanya usafi
maeneo ya kaya zao na kupanda miti minne kila kaya, kulipa ada ya taka sh 2000
na wafanyabiashara sh 5000 kwa mwezi ili kudumisha usafi wa mji na kuboresha
mazingira .
Katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Manispaa ya
Singida ilitangaza kutumia zaidi ya Sh Milioni 701.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya maendeleo ikiwamo ununuzi wa magari ya kuzolea taka fedha ambazo zimetokana
na mapato ya ndani.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa Singida, Serukamba aliwataka Wananchi wa Manispaa ya Singida kuhifadhi takataka wanazo zalisha majumbani mwao badala ya kuzitupa barabarani au kuzipeleka kwenye majalala huku Halmashauri ya Manispaa hiyo ikiagizwa kuweka utaratibu wa kupita kila kaya kukusanya taka hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jeshi Lupembe,
No comments:
Post a Comment