NMB YATENGA BILIONI 200 KWA AJILI YA KUWAKOPESHA WAFANYAKAZI KUPATA ELIMU YA JUU…! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 15 March 2023

NMB YATENGA BILIONI 200 KWA AJILI YA KUWAKOPESHA WAFANYAKAZI KUPATA ELIMU YA JUU…!

 




BENKI ya NMB imetenga kiasi cha TZS bilioni 200 kwa ajili ya kuwakopesha wafanyakazi kupata elimu ya juu au wale wanaohitaji fedha za kuwasomesha wategemezi wao. 

Huduma hio mpya ya mikopo ya elimu ya juu ‘NMB Elimu Loan’ yenye riba nafuu maalum kwaajili ya watumishi na wafanyakazi ambao mishahara yao inapitia benki ya NMB imezinduliwa leo jijini Dodoma. 

Hii inaenda kuleta ahueni kubwa katika ufadhili wa elimu ya juu nchini, na pia itatolewa kwa vyuo vya kati ikiwemo vyuo vya ufundi.

Mpango ni huu:

·         Mkopo unatolewa kwa mwajiriwa yoyote ambae ni mteja wa NMB

·         Unaanzia TZS 200,000 hadi TZS milioni 10 kwa mwaka kwa mtu mmoja

·         Riba ya 9% na muda wa marejesho wa miezi 12

·         Unatolewa pia kwa ngazi ya vyuo vya kati vikiwemo vyuo vya ufundi. 

Akitangaza kuanzishwa kwake rasmi, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi Ruth Zaipuna, alisema 

“Huu ni  utekelezaji wa makubaliano yetu na Wizara ya Elimu ya kuanza kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kupunguza utegemezi wa  waajiriwa kwa bodi ya mikopo (HESLB) pale wanapotaka kujiendeleza kimasomo na pia kuwalipia ada vijana wao,” alifafanua.

Aidha, alisema kuwa NMB ina dhamira ya dhati katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha tasnia ya elimu na kuchangia kutoa elimu bora kwa wote huku ikiwa mstari wa mbele kupanua wigo wa upatikanaji wa fedha za kuwafadhili wote wanaohitaji kujiendeleza kielimu.

“Ili kupata mkopo huu, fika tawi lolote la NMB na nakala ya mshahara wako, mtiriko wa ada, barua ya kujiunga na chuo na wafanyakazi wa Benki ya NMB watakupigia hesabu ya mkopo unaostahili kupata,” CEO Zaipuna alidokeza wakati akiyataja masharti ya kukopeshwa.

Kwa kuanzisha huduma hii, NMB inakuwa imetimiza ahadi iliyoitoa mwaka jana yakuisaidia Serikali kuipunguzia HESLB mzigo wa kufadhili masomo ya juu na kuwa na vyanzo vipya vya mikopo ya elimu. 

Katika hotuba yake, Waziri Mkenda aliweka bayana matamanio yake ya kutaka kupatikana ufadhili zaidi ya kile ilichokifanya NMB kutoka kwa wadau wengine. 

Aidha, alisema kuwa uwekezaji wa NMB ni kitu kikubwa kinachoongeza wigo wa watu kujisomesha na akaomba hela za mikopo hiyo zitumike kwa ajili ya madhumuni yaliyokosudiwa tu. 

Waziri huyo alisema pamoja na bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kuongezeka kutoka TZS bilioni 464 Serikali ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani hadi TZS bilioni 657 kwenye mwaka huu wa fedha bado kuna uhitaji wa vyanzo vingine kama hiki kipya kilichoanzishwa na NMB. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Prof Kitila Mkumbo, alisema uzinduzi wa huduma mpya uliyofanywa na NMB ni muhimu sana kwani fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi hazijawahi kutosha. 

Tembelea tawi lolote la NMB karibu nawe kujipatia huduma hii.




No comments:

Post a Comment