SERIKALI INADHAMIRA YA DHATI KUBORESHA SEKTA YA HABARI NCHINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 18 December 2022

SERIKALI INADHAMIRA YA DHATI KUBORESHA SEKTA YA HABARI NCHINI

Viongozi mbalimbali na washiriki wakiwa kwenye  kongamano la maendeleoya ya sekta ya habari 2022 linaloendelea Ukumbi wa Mikiutano wa Kimataifa  wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaaam.

Na Dotto MwaibaleDar es Salaam

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema Serikali inadhamira  ya dhati ya kuboresha sekta ya habari nchini.

Nape ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la maendeleoya ya sekta ya habari 2022 linaloendelea Ukumbi wa Mikiutano wa Kimataifa  wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaaam.

Alisema serikali ina kila sababu ya kuboresha mazingira bora ya vyombo vya habari kutokana na umuhimu wake hasa katika maendeleo na kuinua uchumi wa nchi.

Nape alisema mwaka ujao wa 2023 Serikali imekusudia kuongeza nguvu zaidi katika kuboresha maslahi ya wanahabari ikiwa ni pamoja na kusimamia mikataba ya ajira zao na kulipwa madeni yao kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo halmashauri za wilaya.

Katika hatua nyingine Nape amevitaka vyombo vya habari kutimiza wajibu kwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na kulinda lasirimali za nchi na pale zinapotumika vibaya waendelee kuwafichua wabadhirifu.

Aliwaomba waandishi wa habari kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali ili kuliletea taifa maendeleo na kukuza uchumi wa nchi na kueleza kuwa kongamano hilolitakuwa endelevu ambapo alipendekeza liitwe kongamano la kimataifa la maendeleo ya sekta ya habari badala ya kongomano la maendeleo ya sekta ya habari.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF) akizungumzia  changangomo kadhaa zinazowakabili waandishi wa habari sambamba na madeni wanayodai  alisema bado kunachangamoto kubwa ya ulipwaji wa madeni hayo.

“Mpaka sasa madeni ambayo vyombo vya habari vinadai kwa serikali na taasisi zake zikiwepo halmashauri ni zaidi ya Sh. 7 bilioni na ukijumlisha  na deni la Gazeti la Daily News la serikali  inakuwa Sh. 11 Bilioni hivyo kulifanya deni lote kufikia Sh. 18 Bilioni ,” alisema Balile.

Katika kongamano hilo Wazri Nape alipata fursa ya kutoa  tuzo kwa waandishi wa babari 10 na taasisi za serikali 10 waliofanya vizuri katika utoaji wa habari na kuandika habari na makala kwenye taasisi hizo ambapo Wizara ya Madini  imetoa tuzo kwa baadhi ya waandishi.

Waandishi waliotunukiwa tuzo hizo ni pamoja na Nelly Mtema (Daily News), George Binagi (BMG Media) na Mohammed Zengwa (Global TV).

Kongamano hilo la siku moja linakutanisha wadau wa habari ikiwa ni pamoja na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari, jukwaa la wahariri wa habari, maafisa habari kutoka Serikalini, Taasisi Binafsi na Mashirika ya Kimataifa. 

Aidha pia katika kongamano hilo zilitolewa mada mbalimbali kutoka kwa Dk. Rose Reuben kutoka TAMWA, Muadhiri wa Dipromasia Deus Kibamba, Kajubi Mkajanga kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT)  Heliet Shija kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkurugenzi Msaidizi wa Idara Habari (MAELEZO) Rodney Tadeus na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dk. Ayoub Ryioba.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akifungua kongamano hilo.

Kongamano likiendelea.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi (kulia) akimkaribisha  akimkaribisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kufungua kongamano hilo.


Waandishi wa habari wakiwa kwenye kongamano hilo.

Msemaji wa Serikali Geryson Msigwa akizungumza kwenye kongamano hilo.

Tuzo zikitolewa kwa waandishi wa habari waliofanya vizuri kuhabarisha umma katika sekta mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Binagi Media GROUP) George Binagi, akikabidhiwa tuzo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye.

Tuzo zikitolewa.

Tuzo zikiendelea kutolewa.

Msema wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna wa Polisi David Misime akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Tuzo ikitolewa kwa wawakilishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni washindi wa utoaji wa taarifa kati ya taasisi 10zilizotunukiwa tuzo na Waziri Nape.

No comments:

Post a Comment