JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa taarifa kwa Vyombo vya Habari kuwa litafanyika zoezi la kawaida la Medani katika maeneo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara kuanzia tarehe 19 hadi 29 Oktoba, 2022.
“Zoezi hilo litahusisha zana vita mbalimbali zikiwemo Ndege vita, Helikopta, Makombora ya masafa ya kati na masafa mafupi, Mizinga ya kutungulia ndege pamoja na zana nyingine”
“Ufunguzi rasmi wa zoezi hilo utafanyika tarehe 22 Oktoba, 2022 saa mbili kamili (2:00) asubuhi katika eneo la Mitwelo Mkoani Lindi. JWTZ linatoa mwaliko kwa Vyombo wya Habari kushiriki kwenye ufunguzi huo”
“Usafiri kwa Wanahabari kuwapeleka eneo la ufunguzi wa zoezi na kuwarejesha utakuwepo saa moja kamili (1:00) asubuhi kona ya Sokoni karibu na Benki ya CRDB, JWTZ linawataarifu Wananchi wa Mikoa hiyo kuwa zoezi hilo ni la kawaida la kujiweka katika hali ya utayari wa kuilinda nchi yetu”
No comments:
Post a Comment