MWANAMITINDO TANZANIA KUSHIRIKI ONYESHO KUBWA LA TUBINGEN, UJERUMANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 12 August 2022

MWANAMITINDO TANZANIA KUSHIRIKI ONYESHO KUBWA LA TUBINGEN, UJERUMANI


Na Zainabu Hamisi, Ujerumani

YALE maonyesho makubwa ya 15 'International Afrika Expo Festival' Tubingen 2022,Ujerumani, yanatarajiwa kuanza mwanzoni mwa September 1 hadi 04 September 2022 katika viwanja vya maonyesho Fest Platz mjini Tuebingen, nchini Ujerumani.

Wasanii na wajasiliamali mbalimbali kutoka nchini Tanzania ndio wanaongoza kwa wingi katika kushiriki maonyesho hayo makubwa ya Kiafrika barani ulaya. Mojawapo wa watakao nogesha maonyesho hayo ni mwanamitindo mbunifu wa mitindo rafiki wa mazingira Bi DIANA JOHN MAGESA ambaye mara nyingi amewai kuipeperusha bendera ya Tanzania katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week, African Fashion Week Canada, UNESCO chini Ufaransa. 

Wasanii wa sanaa za maonyesho na wajasiliamali mbalimbali kutoka moja kwa moja nchini  Tanzania wanatarajia kuonyesha kazi zao katika maonyesho hayo nchini Ujerumani. 

KARIBUNI UJERUMANI

https://www.africafestival-international.org

No comments:

Post a Comment