Ugeni wa Wanajeshi kutoka Zimbabwe wakifuatilia filamu ya The Royal Tour Tanzania. |
Ugeni huu unaongozwa na Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Zimbabwe, Kanali C. Kaondera ambaye ameambatana na Wakufunzi wengine name (8) pamoja na Wanafunzi kumi na nnne (14) kutoka katika nchi za Zimbabwe, Afrika Kusini pamoja na Lesotho.
Katika ziara yao ya siku kumi (10) wameweza kutembelea ofisi za TTB ambapo wamepata taarifa mbalimbali za utalii kwa kina pamoja na kuangalia filamu ya The Roya Tour Tanzania” ambayo ilionyesha kuwavutia sana na kuwafanya watamani kuyatembelea maeneo ya vivutio yaliyooneshwa kwenye filamu hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Dkt. Gladstone Mlay amesema “tumefarijika kuona nchi wanachama wa SADEC wanakuja nchini kwetu kujifunza, tutaendelea kushirikiana kwa pamoja kuvitangaza vitutio vyetu vya nchi wanachama ili tuweze kuviuza kwa pamoja. Tunaendelea kuwahamasisha watalii kutoka sehemu nyingine waweze kupanga safari zao za mapumziko kutembelea zaidi ya nchi moja za kusini mwa Afrika”.
Kwa upande wa Zimbabwe, Kanali C. Kaondera amesema “ziara yetu hii tumejifunza mengi kuhusiana na utalii wa Tanzania hasa kauli mbiu ya “Tanzania Unforgettable” na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa kushawishi wananchi wa Zimbabwe kuja kuvitembelea vivutio vya Tanzania. Hii haitakuwa safari yetu ya mwisho, tutakuja tena ili tuweze kutembelea maeneo mengine”
Naye Kanali Babuu kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambaye ndiyo mweji wa ugeni huu amesema” Wageni wamefurahishwa sana na hali ya ulinzi na usalama iliyopo inchini Tanzania, kwani wameweza kutembea nyakati za jioni na kurudi kwenye makazi yao wakiwa salama. hivyo, tujiandae kupokea watalii wengi zaidi kutoka nchi wanachama wa SADEC.
No comments:
Post a Comment