Viongozi wa HLI kutoka Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda, katika Kikao na Mbunge wa EALA, Mh, Pamela Maasay, Kikao hicho kilifanyika katika ofisi za Bunge la EALA jijini Arusha. |
SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Uhai Tawi la Afrika Mshariki (HLI) limedhamiria kutengeneza Waraka unaoeleza maovu na mapungufu yaliyoko kwenye Muswada wa Ujinsia na Afya ya Kizazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Mwaka 2020/2021.
Waraka huo pia utaeleza namna ya kurekebisha Muswada huo ili uendane na hali halisi ya Maisha ya Wananchi wa Jumuiya katika kujali Utu, Imani na Mila na tamaduni zao.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa HLI Kanda ya Afrika kwa Nchi zinzozungumza Lugha ya Kingereza, Emily Hagamu anasema Wakara utakapokamilika utawasilishwa kwenye Kamati ya Malengo ya Jumla, (General Purpose) ya Bunge la Jumuiya ya Afrika kabla ya Vikao vyake vya Maoni ya Jumla ambavyo vinatarajia kuanza Julai 22 mwaka huu.
Mbali na hatua hiyo, (HLI) inakusudia pia kuaandika andiko lenye Malalamiko yakionyesha Uovu wa Muswada huo na mchakato wake mbovu ambayo yatasainiwa na Wananchi wa Jumuiya hiyo, ikiwa ni hatua ya kukusanya kura kutoka kwa Wananchi za kupinga Vipengele vya Uovu vilivyoko kwenye Muswada huo.
Kwa mujibu Hagamu, andiko hilo litawasilishwa kwa Sipika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, (ELA) Mh, Martin Ngoga.
Viongozi hao pia wamekubaliana kuunda timu ya Wawakilishi kutoka katika Nchi zao, ambapo watakuwa wakikutana nao na kuwajengea uwezo wa kina katika kutambua Vipengele vyenye Uovu ndani ya Muswada huo.
"Mfano wa Kipengele cha Uovu katika Muswada huo ni kile kinachosema Vijana na Watoto wawe na Uwezo kupata Huduma za Ujinsia na Haki ya Kizazi kwa Uhuru bila kushurutishwa na wasipate kwa Siri," Alisema Hagamu.
Anasema Kipengele hicho kinakwenda kinyume na tamaduni za Watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani, Watoto na Vijana katika malezi wanawajibika kwa Wazazi.
No comments:
Post a Comment