MAFANIKIO MENGI YA URUSI YAZUIWA DONBAS - UINGEREZA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 20 April 2022

MAFANIKIO MENGI YA URUSI YAZUIWA DONBAS - UINGEREZA

 

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky.

'Tungemaliza vita iwapo Ukraine ingekuwa na silaha bora' anasema Rais Zelensky.

Katika hotuba yake ya mara kwa mara katika kanda ya video kwa taifa lake, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kwamba iwapo Ukraine ilikuwa ikimiliki silaha bora ikilinganishwa na zile za Urusi , ingekuwa imemaliza vita.

Rais Zelensky alisema kwamba katika mahojiano yake na majadiliano na viongozi wa mataifa yaliopiga hatua kubwa kidemokrasia, ‘’sio haki kwa Ukraine kuendelea kuomba usaidizi wa kile ambacho washirika wake wamekuwa wakihifadhi kwa miaka kadhaa’’.

Alisema kwamba iwapo mataifa hayo yanamiliki silaha ambazo Ukraine inahitaji ni jukumu lao kusaidiakulind na kuokoa maisha ya maelfu ya raia wa Ukraine.

Aliongezea kwamba iwapo taifa lake lingefanikiwa kupata silaha hizo ambazo wameahidiwa wiki zijazo, zingesaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watu.

Rais aliongezea kwamba uwezo wa mashambulizi ya Urusi katika maeneo ya Kharkiv, Donbasna Dnipropetrovsk umeongezekana hata kulenga makaazi ya raia.

‘’Hatma ya makumi ya maelfu ya wakaazi wa Mariupol ambao walipelekwa katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi haijulikani’’, alisema Zelensky’’.

Hatua hii inajiri huku wizara ya ulinzi ya Urusi ikitoa masharti mapya kwa wanajeshi wa Ukraine waliozungukwa katika mji wa Mariupol kusalimu amri.

Utawala wa Biden unapanga kutangaza kifurushi kingine cha msaada wa kijeshi wenye thamani ya $800m (£615m) kwa Ukraine, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Alipoulizwa Jumanne huko Portsmouth, New Hampshire, ikiwa angetuma silaha zaidi kwa Ukraine, Rais Biden alijibu: "Ndiyo."

Ikulu ya White House wiki iliyopita ilitangaza kutuma msaada wa kijeshi wa thamani ya $800m kwa Ukraine ambao utajumuisha raundi 40,000 za mizinga na Howitters 18 (155mm.)

No comments:

Post a Comment