Mafunzo yakiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Singida
CHAMA cha Girl Guides Tanzania (TGGA) kimetoa mafunzo kwa walimu kutoka shule za Sekondari na Msingi katika Halmashauri za wilaya tatu mkoani Singida yaliyowalenga wasichanaa na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Mafunzo hayo yaliwahusisha walimu na wanajamii kutoka katika Halmashauri za wilaya yaIkungi, Singida DC na Manispaa.
Akizungumzia mafunzo hayo Afisa Mradi Msaidizi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi na Mazingira kutoka TGGA, Praxeda Swai alisema mafunzo hayo ya siku nne yamewalenga walimu hao na wasichana ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na masuala ya tabia nchi na kugombea uongozi.
“Baada ya kuwapatia mafunzo haya walimu na wanajamii ambao tumewakutani hapa wataenda kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kuchukua hatua chanya cha kukabiliana na changamoto za tabia nchi akitolea mfano Mkoa wa Singida ambao ulikuwa ukikabiliwa na ukame kutokana na ukataji wa miti” alisema Swai.
Alisema kazi kubwa watakayokuwa wakiifanya ni kuhamasisha jamii kupanda miti kwani wahanga wakubwa kunapokuwa na ukame ni wasichana na mama zao ambao wanakuwa wakiangaika kwenda kutafuta maji wakitumia muda mwingi na umbali mrefu na kuwa lengo lao ni kuifanya Singida kuwa ya kijani.

No comments:
Post a Comment