NMB YASAINI MAKUBALIANO NA SMZ KUBORESHA UKUSANYAJI MAPATO YA UTALII - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 21 January 2022

NMB YASAINI MAKUBALIANO NA SMZ KUBORESHA UKUSANYAJI MAPATO YA UTALII

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk Khamis wakibadilishana nyaraka za mkataba mara baada ya kusaini mkataba kushirikiana katika kuimarisha na kukuza ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya utalii visiwani.


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk Khamis wakisaini mkataba kushirikiana katika kuimarisha na kukuza ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya utalii visiwani.



BENKI ya NMB imesaini makubaliano ya kimkakati na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushirikiana katika kuimarisha na kukuza ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya utalii visiwani humo kupitia mifumo ya kidijitali.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk Khamis.

Kupitia ushirikiano huu, Benki ya NMB itachagiza shughuli za kitalii kupitia; Kuwekeza kwenye mfumo wa kidigitali utakaotumika kufanya makusanyo ya Serikali katika vituo vyote vya utalii Zanzibar.

Kusambaza mashine za malipo (POS) kwenye vituo vya makusanyo na vivutio vya utalii. Hii itawawezesha watalii kulipia ada na tozo zote kupitia kadi zao za Mastercard, Visa na UnionPay.

Kutoa elimu na kuhamasisha watu kuzidi kutembelea vivutio vya kitalii vilivyopo visiwani humo kupitia matamasha na promosheni mbali mbali.

#NMBKaribuYako

No comments:

Post a Comment