MHE. MCHENGERWA AJA NA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE SANAA NA MICHEZO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 15 January 2022

MHE. MCHENGERWA AJA NA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE SANAA NA MICHEZO

Hafla ya fainali za mashindano ya sanaa ya Bongo Star Search (BSS) msimu wa 12 jijini Dar es Salaam ikiendelea.

Washindi wa fainali za mashindano ya sanaa ya Bongo Star Search (BSS) msimu wa 12 jijini Dar es Salaam wakipokea zawadi zao.

Washindi wa fainali za mashindano ya sanaa ya Bongo Star Search (BSS) msimu wa 12 jijini Dar es Salaam wakipokea zawadi zao.

Washindi wa fainali za mashindano ya sanaa ya Bongo Star Search (BSS) msimu wa 12 jijini Dar es Salaam wakipokea zawadi zao.

Na John Mapepele- WUSM

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa amesema Wizara yake itahakikisha inafanya kazi kuanzia ngazi ya mitaa na vijiji  ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta hizo katika kipindi kifupi.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo usiku wa Januari 14, 2022 kuamkia leo akiwa Mgeni Rasmi kwenye fainali za mashindano ya sanaa ya Bongo Star Search (BSS) msimu wa 12 jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi, na Naibu Katibu Mkuu, Said Yakubu.

 "Tunataka tuizungumze sanaa katika kila mtaa, tutaizungumza Sanaa katika kila kata, tutaizungumza Sanaa katika kila wilaya, na tutaizungumza Sanaa katika kila mkoa, tunataka Sanaa ndiyo iwe msingi katika kulinda na kuendeleza  utamaduni wa taifa letu" amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanakwenda  kufanya mageuzi katika sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Aidha,  amesisitiza kuwa yeye ni mtu wa kasi katika utendaji na matokeo zaidi hivyo atahakikisha kuwa  matokeo makubwa yanapatikana katika Wizara yake.

Mhe. Mchengerwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi kuona uwezekano wa kuwaendeleza washiriki wote wa shindano hilo katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo kilicho chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza ni Bryson Yohana kutoka Dar es Salaam, mshindi wa pili ni Andrew Charles kutoka Mwanza na mshindi wa tatu ni Suleiya Abdi mwanadada kutoka mkoa wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment