MBUNGE TAWHEEDA ANOGESHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 45 CCM -UWT WILAYA YA SINGIDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 29 January 2022

MBUNGE TAWHEEDA ANOGESHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 45 CCM -UWT WILAYA YA SINGIDA

Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) ambaye alikuwa mgeni rasmi, akizungumza katika Maadhimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida DC yaliyofanyika juzi mkoani Singida. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, William Nyalandu.

Mwenyekiti wa  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida DC Neema Sambaa akimvika  vazi la kimila la kabila la Wanyaturu Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) ikiwa ni kumpa heshima wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia alikabidhiwa kibuyu cha jadi cha kabila hilo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) (kulia) muda mfupi baada ya kuwasili wilayani Singida DC kwenye maadhimisho hayo.
Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) akizungumza na Wanawake wa UWT Wilaya ya Singida DC.
Burudani zikiendelea na mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.
Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) akigawa  zawadi kwa watoto. Kulia ni Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida DC Naomi David
Shamra shamra kwenye maadhimisho hayo zikiendelea ambazo zilifanyika sambamba na kumpa zawadimgeni rasmi.
Maadhimisho yakiendelea.
Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) akipanda mche wa mti katika viwanja vya ofisi ya UWT wakati wa maadhimisho hayo.


Na Mwandishi Wetu 


MBUNGE wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) amewataka Wanawake  kufanya kazi kwa bidii  na kwa  kujiamini pamoja na kuondoa dhana ya kwamba wao hawawezi kuongoza kwa kuwa ni mwanamke kwani  mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi.

Hayo aliyasema  wakati wa maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyoadhimishwa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Singida (UWT)

Mhe Tawheda alisema kwa sasa nchi yetu inaongozwa na mwanamke na  anatuongoza vizuri sana! Anatimiza hamu na kiu ya watanzania, analiendesha gurudumu la maendeleo vizuri kwa maslahi mapana ya watanzania.  

"Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi makini na mwenye uwezo mkubwa na  ameudhihirishia ulimwengu  kwamba wanawake tunacho kipaji cha kuongoza licha ya kuwa na majukumu  mengi tuliyonayo ya kifamilia lakini tunapokuwa na jukumu la kuongoza tunalifanya kwa ufanisi mkubwa na kuhakikisha malengo yanatimia" alisema Garlos.

Aliwataka Wanawake kuiga mfano wa mhe Rais Samia Suluhu Hassan ambaye  anachapa kazi kwa juhudi na  weledi mkubwa.

Katika maadhimisho hayo  mhe Tawheeda alitembelea Kituo cha Afya cha Ilongero cha Wilaya ya Singida  na kujionea jinsi kinavyotoa huduma pamoja na  kuona changamoto zake na kuahidi kushirikiana na wabunge wa Singida kuzisemea  ambapo pia alipata nafasi ya kuwaona wagonjwa  na kuwapa zawadi  kwa lengo la kuwafariji.

Awali Mbunge Tawheeda alipowasili ofisi za chama alilakiwa na viongozi wa chama wa UWT na Jumuiya ya Wazazi wilayani humo wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo William Nyalandu  na baadaye alipata fursa ya kupanda mti katika ofisi ya chama wilaya   na kuongoza Harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya mtendaji wa chama. 

Miongoni mwa shughuli alizozifanya akiwa wilayani humo ni kugawa kadi kwa wanachama wapya zaidi ya 100 waliojiunga na CCM. 

Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa  na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mhe.Ramadhani Ighondo na Mhe.Aysharose Mattembe Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.

Viongozi wengine waliokuwepo ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Singida DC, Anthony Katani. Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Wazazi Wilaya Singida Alexander Mbogho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT  Wilaya ya Singida DC Neema Sambaa na Katibu wa UWT wilaya Naomi David.

No comments:

Post a Comment