Muonekano wa daraja la waenda kwa miguu lililopo Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani (Magufuli Terminal) katika barabara ya Morogoro sehemu ya Mbezi, jijini Dar es Salaam. |
Muonekano wa Barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara – Kibaha (njia nane), ambayo ujenzi wake unaendelea jijini Dar es Salaam. |
Muonekano wa Barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara – Kibaha (njia nane), ambayo ujenzi wake unaendelea jijini Dar es Salaam. |
NAIBU Waziri wa Ujenzi
na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),
Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha maboresho yanayofanywa katika ujenzi wa
barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara – Kibaha (njia nane), yanakamilika
ifikapo Juni mwaka huu.
Akizungumza mara baada
ya kukagua maendeleo ya Ujenzi huo, Eng. Kasekenya amewataka wataalam
wanaosimamia maboresho ya barabara hiyo waendelee na zoezi la utoaji elimu kwa
madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo ili kupunguza ajali.
“…TANROADS
shirikianeni na askari wa usalama barabarani kutoa elimu ya namna bora ya
kutumia vivuko vya juu na chini ya barabara pindi ujenzi wake unapokamilika na kuhakikisha
barabara zinakuwa safi wakati wote,” amesema Naibu Waziri Eng. Kasekenya.
Amewaonya wote
wanaoharibu alama za barabara na kutupa taka ngumu kuacha mara moja uharibifu
huo na kuwataka wasimamizi wa barabara kuwachukulia hatua za kisheria mara
moja.
Kwa upande wake, Meneja
wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dar es Salaam, Eng. Harun
Senkuku amemhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa
barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara – Kibaha (njia nane), yenye urefu wa KM
19.2, uliohusisha madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji umekamilika na
kinachoendelea sasa ni uboreshaji wa njia ya mwendokasi katika barabara hiyo.
Aidha amezitaja kazi nyingine
zinazoendelea kwa sasa kuwa ni ujenzi wa madaraja mawili ya juu eneo la Mbezi
Mwisho na Kwa Yusuf kwa ajili ya kupunguza msongamano katika Kituo Kikuu cha
Mabasi ya Mikoani cha Magufuli, kujenga barabara ya maingilio katika kituo
hicho, kujenga kituo cha mabasi ya daladala eneo la Kibamba njia ya Mloganzila na kuongeza taa za
kuongozea magari eneo la makutano ya barabara ili kurahisisha uvukaji wa magari
na watembea kwa miguu.
Takribani kiasi cha
shilingi bilioni 218, zinatarajiwa kutumika katika mradi huo hadi utakapo
kamilika baadaye mwezi juni mwaka huu.
Imetolewa na Kitengo
cha Habari na Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment