DKT. ABBASI: TUTAIONESHA DUNIA UTAMADUNI WETU KUTOKEA MOSHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 20 January 2022

DKT. ABBASI: TUTAIONESHA DUNIA UTAMADUNI WETU KUTOKEA MOSHI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akizubgumza.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi,  Januari 20, 2022, amekagua maandalizi ya Tamasha kubwa la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro.

Katika Tamasha hilo litakalofanyika Januari 22, 2022, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Chifu, akitumia jina la Chifu Hangaya. 

“Maandalizi yanakamilika na tayari vikundi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huu vinaendelea na mazoezi na wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania wameendelea kuwasili hapa Moshi.

“Tamasha hili linafungua njia ya matamasha mengine ya Utamaduni  wetu kuendelea hapa nchini. 

Tunataka kutumia utamaduni na sanaa kuileta dunia na kuionesha dunia kile Tanzania ilichonacho,” amesema Dkt. Abbasi kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.

Tamasha hilo limeandaliwa na machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Chifu Frank Marealle na kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

No comments:

Post a Comment