| Balozi, Profesa Abillah Harrid Omary Mgeni rasmi katika mahafali hayo akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo hicho. |
| Wahitimu wakifuatilia tukio la utunukishwaji wa vyeti wakati wa hafla ya mahafali yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo Kikuu cha Kampala Dar es Salaam. |
Na Dunstan Mhilu
WAHADHIRI Nchini wametakiwa kufanya tafiti na kutoa machapisho ya kutosha kwa ajili ya kufundishia ili kuepuka kukaririsha wanafunzi.
Hayo yalielezwa jana na Balozi, Profesa Abillah Harrid Omary wakati wa kuwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIUT) katika mahafali ya nne yaliyofanyika katika chuo hicho Gongolamboto Dar es Salaam.
Balozi, Profesa Abillah alimuwakilisha Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi kama mgeni rasmi na kueleza kuwa kuna kila sababu ya wahadhiri kujielekeza kwenye tafiti kwakua ndiyo nyenzo zinazozaa ufahamu.
“Kiongozi mmoja wa China aliwahi kusema ‘Hakuna utafiti,hakuna haki ya kusema, viongozi wetu wa Chuo nanyi muwe chachu katika hili muongeze juhudi za kutafuta fedha zakufanyia tafiti kwakuwasiliana na wafadhili, Taasisi na Makampuni” alisema
Vilevile Balozi, Profesa Abillah alisema wataendelea kufanya kazi bega kwa bega na serikali katika kuunga kauli mbiu ya Rais Samia Suluhu Hassan ‘Kazi Iendelee’
“Nawaomba wote tumuombee Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake na sisi tunaunga mkono kauli mbiu yake kwakuchapa kazi ka maarifa na juhudi ili kuzalisha wataalamu wenye weledi watakao litumikia Taifa.
Hata hivyo alitoa mwito kwa wahadhiri kukubali kukoselewa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kwani katika utoaji wa elimu ya juu duniani kote hakuna njia ya mkato na Taasisi hiyo ipo kwa ajili ya kusimamia ubora wa elimu nchini.
“Napenda kutoa mwito kwa uongozi wa Chuo tusibeze, kukosolewa na kuhakikiwa na TCU,tusimchukie anyaetupa tahadhari ya mbele” alisema Balozi Profesa Abillah
Pia aliwataka wahitimu hao wakaonyeshe tofauti chanya kwa kuwa waaminifu na waadilifu na kutoshiriki Kwa namna yeyote ile katika matendo ya kifisadi ili kutetea na kulinda maslahi ya Taifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza wa chuo hicho, Profesa,Yunus Mgaya aliwataka wahitimu hao waende kuwa kiungo mahususi kati ya jamii na maendeleo hivyo matatizo na mafanikio wanayopitia si yao pekee bali ni kwa manufaa ya jamii yote.
"Baraza letu limeendelea kuimarisha mifumo mbalimbali muhimu kwa ajili yakutoa miongozo, kusimamia na kuimarisha utendaji kazi wa Chuo hiki"alisema Profesa Mgaya
Naye Naibu Makamu wa Chuo hicho,Profesa Angwara Kiwala alisema Chuo hicho kilizuliwa kusajili wanafunzi kwa sababu ya upungufu katika maeneo mbalimbali ya uendeshaji wa chuo hivyo baada ya maboresho hayo kwa mujibu wa maelekezo ya miongozo ya TCU udahili wa wanafunzi kwa programs umekuwa ukifungiliwa Kwa awamu lakini sasa wameruhusiwa kufundisha kozi zote baada ya TCU kujiridhisha.
"Kwa mwaka wa masomo2021/2022 Chuo chetu kimeweza kusajili jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza 3,144 na ninatoa shukrani kwa TCU na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(Nacte) kwa ushauri na miongozo waliotupatia kwa umekuwa mchango mkubwa hadi kufikia mafanikio makubwa kitaaluma leo hii ambapo program zote zilizopangwa kutolewa na chuo hiki sasa zitatolewa pasina shaka”alisema
Wahitimu hao wametakiwa kutochagua kazi , kwakuwa ajira zinapatikana kwa shida, vilele wmeshauriwa kujitolea katika Kampuni, Taasisi na Mashirika mbalimbali nchini kama njia ya kujipatia ajira kiurahisi.

No comments:
Post a Comment