Na Projestus Binamungu, WUSM
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa
ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kushirikiana na Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) kuhakikisha wanaiwekea mazingira wezeshi timu ya Taifa
ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 Tanzanite yatakayowajenga kimwili na
kisaikolojia wachezaji hao katika kuikabili timu ya taifa ya Ethiopia January
2022.
Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo Desemba 21,
2021 alipokutana nao na kufanya mazungumzo na wachezaji pamoja na kamati ya
ufundi ya timu hiyo kujadili na kufanya tathimini ya changamoto mbalimbali za
kimichezo zilizojitokeza wakiwa nchini Burundi wakati wa mchezo baina ya
Tanzanite na wenzao wa timu ya wanawake ya Burundi ya chini ya umri wa miaka
20.
Waziri Bashungwa amesema kazi ya Serikali
katika sekta ya michezo ni kuweka mazingira wezeshi kwa wanamichezo na timu
zote zinazoipeperusha bendera ya taifa, na ndoto ya Serikali ni kuwaona
wachezaji na timu zao wakiibuka washindi katika michezo yote.
Pamoja na kuelezea matamanio hayo ya Serikali,
Waziri Bashungwa ameipongeza timu ya Tanzanite katika mchezo wao dhidi ya
Burundi uliochezwa Desemba 18, 2021 na kuibuka na sare ya bao moja licha ya
kucheza wakiwa pungufu.
“Kwa kweli mliishangaza Afrika na dunia huko
Burundi, yaani mnacheza pungufu lakini bado tukapata ushindi wa heshima, kwa
kweli tunawapongeza sana vijana wetu,” amesema Waziri Bashungwa.
Awali akielezea baadhi ya changamoto
walizokabiliana nazo huko Burundi, Mkuu wa msafara wa timu ya Tanzanite Bukuku
Mrisho amesema, licha ya sheria za mpira kutaka majibu ya vipimo vya magonjwa
mbalimbali kuwasilishwa masaa mawili kabla ya mchezo lakini wao waliletewa
majibu ya vipimo vya Uviko 19 wakiwa uwanjani tayari na hata wakati mchezo
ukiendelea wataalamu waliendelea kuleta majibu ya vipimo kwa viongozi
mbalimbali wa timu.
“Yaani wakati mchezo unaendelea waliendelea
kutuletea makaratasi waliyo ya kuandikwa kwa mkono kwamba fulani majibu
yanaonesha ana Uviko 19, sisi tunaamini nia yao ilikuwa ni kututoa mchezoni
lakini tulipambana na upungufu wetu huo huo mpaka mwisho wa mchezo tukaibuka na
sare ya goli moja,” amesema Mrisho.
Tanzinite inashiriki michezo hiyo ya awali
kupata tiketi ya kufuzu kushiriki mashindano ya kombe la dunia yanayotarajiwa
kufanyika mwaka 2022 nchini Costa Rica.
Amekuja kufanyamajadiliano nakubadilishana uzoefu katika sekta ya mawasiliano, Tanzania na Rwanda ni nchi ambazo zimekuwa na ushirikiano kwa muda mrefu kupitia Shirika la Mawasiliano la Tanzania na lile la Rwanda na mahusiano ya kibiashara. TTCL ni moja ya wadau anayepeleka mawasiliano katika nchi ya Rwanda na amekuwa akitoa mawasiliano hayo takribani miaka 10 sasa, hivyo nimemkaribisha Waziri kwanza aje kuona sehemu ambayo mawasiliano yake ya nchi ya Rwanda yanapita na pili kuja kubadilishana uzoefu kwa pande zote mbili.
“..Nchini kwetu hii ni Wizara Mpya (Tehama) na kwa Rwanda kuna hatua ambazo wamepiga katika maendeleo ya Tehama, lakini pia kuja kuangalia fursa zinazopatikana Tanzania na sisi kuangalia fursa hizo kwa nchi ya Rwanda.
Alisema katika ziara hiyo Waziri wa Rwanda na Tanzania watafanya majadiliano kuangalia maeneo ambayo wanaweza kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuboresha zaidi mahusiano kati ya pande zote.
No comments:
Post a Comment