T-PESA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA NA SHIRIKA LA POSTA TANZAINA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 7 December 2021

T-PESA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA NA SHIRIKA LA POSTA TANZAINA

Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (wa pili kushoto) pamoja na Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel (wa pili kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), kwa makubaliano hayo kwa sasa TPC inakuwa WAKALA MKUU ambaye anaenda kubeba dhamana ya kuwahudumia MAWAKALA WADOGO wa T-PESA.



Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) pamoja na Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel (kulia) wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde akizungumza kwenye hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), leo jijini Dar es Salaam.


Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel akizungumza kwenye hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (katikati aliyesimama) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kwenye hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (wa pili kushoto) na Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel (wa pili kulia) wakionesha nakala za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kibiashara baina ya pande mbili. Pembeni yao ni wanasheria wa pande zote mbili wakishuhudia.

Na Mwandishi Wetu, Dar

KAMPUNI ya T-PESA imeingia makubaliano ya ushirikiano kibiashara na Shirika la Posta Tanzaina (TPC) unaolenga kurahisisha huduma za kifedha kwa mawakala pamoja na wateja wake.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mpango wa T-PESA kuboresha huduma zake za Kifedha nchini na kuhakikisha wateja wake wanakuwa karibu zaidi na mawakala na pia kupata huduma kwa urahisi, haraka na kwa bei nafuu.

Aidha alisema katika makubaliano hayo kwa sasa Shirika la Posta linakuwa WAKALA MKUU ambaye anaenda kubeba dhamana ya kuwahudumia MAWAKALA WADOGO. Alisema T-Pesa inatambua ukubwa wa Shirika la Posta na mchango wake katika kutoa huduma kwa wananchi, hivyo kitendo cha Posta kupewa nafasi hiyo ni chaguo sahihi kuwafikia mawakala wadogo na wateja hadi ngazi ya wilaya. 

"...Kwa nafasi ya kipikee napenda kuishukuru Menejimenti ya Posta chini ya Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Mbodo kwa kukubali Shirika la Posta kuwa WAKALA MKUU ambaye anaenda kubeba dhamana kubwa ya kuwahudumia MAWAKALA WADOGO. 

Tunatambua ukubwa wa Shirika la Posta na mchango wake katika kutoa huduma kwa wananchi. Tunahakika POSTA kuwa WAKALA MKUU ni chagua sahihi ya kuwafikia mawakala wadogo na wateja hadi ngazi ya Wilaya," alisema Bi. Lulu Mkudde.

Aliongeza kuwa T-PESA inaendelea na uboreshaji wa huduma zake huku lengo likiwa ni kuhakikisha huduma zinapatikana kwa urahisi zaidi mahali popote na ndiyo haswa sababu ya kuendelea kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na taasisi zingine.

Akifafanua zaidi kwa wanahabari, Bi. Mkudde alibainisha kuwa muunganiko huo wa huduma za kibiashara baina ya taasisi hizo mbili unalenga kuwawezesha wananchi kufanya miamala yao ya Kifedha kwa njia rahisi na salama zaidi, ambapo sasa Wakala wa T-PESA atakuwa na uwezo wa kupata Floti kupitia POSTA ikiwemo huduma za Uwakala kwa Wateja kutoa pesa kwenye akaunti zao kupitia Ofisi za TPC.

"...Ili kufanikisha ukuaji wa huduma zitolewazo na T-PESA, mipango madhubuti imekuwa ikifanywa ikiwa ni pamoja na kuunganisha huduma zetu pamoja na benki mbalimbali ikiwemo CRDB, TCB, (zamani TPB), NMB, Peoples Bank of Zanzibar na AZANIA Benki ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zetu," aliongeza Bi. Mkudde.

Kwa upande wake, Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel akizungumzia katika hafla hiyo alisema ushirikiano huo baina ya T-PESA na TPC utaleta tija kwa pande zote mbili kutokana na kwamba huduma zao zimesambaa nchi nzima na sasa huduma za T-PESA zitapatikana kila mahali zilipo huduma za Shirika la Posta.

No comments:

Post a Comment