DKT. ABBASI AWATAKA WASANII KUIPA HESHIMA TASNIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 28 November 2021

DKT. ABBASI AWATAKA WASANII KUIPA HESHIMA TASNIA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amewataka wasanii nchini kushiriki  kuiendesha tasnia kwa weledi, kujenga umoja na kuiongezea thamani wao wenyewe kwakutoa maoni ya kuboresha kila eneo badala ya kuwa walalamikaji miaka nenda rudi.

Dkt. Abbasi amesema hayo Novemba 28, 2021, jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wadau wa tasnia ya filamu nchini katika hatua za kujipanga zaidi kuelekea Tamasha la Tuzo za Filamu za mwaka 2021 ambazo Serikali kupitia Bodi ya Filamu imeamua kuzirejesha na zitafanyika mwaka huu kwa mara ya kwanza wakati pia tuzo za muziki na sanaa nyingine nazo zikiwa jikoni.

Amewasisitiza wasanii kuthamini tuzo hizo kwa kuwa zinalenga kuwatangaza ndani na nje ya nchi pamoja na kuwapa hamasa ya kufanya kazi bora zaidi.

“Penye kasoro tuambieni tutaboresha, ukikosa tuzo usinune angalia ulipojikwaa mwakani ufanye vyema zaidi lakini kwa ujumla tuzo hizi ni za nchi wala sio za mtu kwa hiyo tutasimamia haki na weledi,” alisema Dkt. Abbasi kauli ambazo zimeungwa mkono nawadau hao wengi.

No comments:

Post a Comment