TUTAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA UCHUKUZI PROF. MBARAWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 9 October 2021

TUTAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA UCHUKUZI PROF. MBARAWA

Muonekano wa mizani mpya ya kisasa inayopima magari yakiwa katika mwendo (weigh in motion), ya Kimokouwa wilayani Longido mkoani Arusha ambayo iko katika hatua za mwisho za kukamilika kwake.

Muonekano wa mizani mpya ya kisasa inayopima magari yakiwa katika mwendo (weigh in motion), ya Kimokouwa wilayani Longido mkoani Arusha ambayo iko katika hatua za mwisho za kukamilika kwake.


WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amemwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Arusha, Eng. Reginald Masawe kuhakikisha ujenzi wa mizani ya kisasa ya Kimokouwa iliyoko wilayani Longido unakamilika haraka.

Mizani hiyo ya kisasa itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kupima magari yakiwa katika mwendo (weigh in motion), na hivyo kuondoa msongamano wa magari katika mpaka wa Namanga unaounganisha Tanzania na Kenya.

“Wiki sita zitawatosha kukamilisha kila kitu na kazi ianze ili kuondoa msongamano na kero kwa wasafirishaji ”, amesema Prof. Mbarawa.

Mradi huo unaojengwa na kampuni ya CRJE ya China na kusimamiwa na Ambicon ya Dar es Salaam utakapokamilika utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 14.7   na unatarajiwa kutoa fursa nyingi za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa wilaya ya Longido.

Amewataka wote watakaopewa nafasi katika mradi huo kufanya kazi kwa bidii, nidhamu, uzalendo na kuepuka vitendo vya rushwa.

Naye Mbunge wa Longido Dkt. Stephen Kiruswa amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa za ajira na biashara ili kukuza uchumi wao.

Amewataka wakazi hao kulinda na kuitunza miundombinu inayojengwa na Serikali kwani hutumia gharama kubwa.

Ujenzi wa mizani ya Kimokouwa  ya kupima magari yakiwa katika mwendo (weigh in motion), ni mkakati wa Serikali kupunguza msongamano katika maeneo yote ya mizani hususan mipakani ili kuharakisha huduma za usafiri na uchukuzi nchini.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI


No comments:

Post a Comment