KM DKT. JINGU AFUNGUA KIKAO KAZI KUANDAA MPANGO KAZI WA TAIFA MASUALA YA WANAWAKE NA ULINZI WA AMANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 27 October 2021

KM DKT. JINGU AFUNGUA KIKAO KAZI KUANDAA MPANGO KAZI WA TAIFA MASUALA YA WANAWAKE NA ULINZI WA AMANI

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu akifungua kikao cha Kikosi kazi cha kuandaa Mpango kazi wa Kitaifa wa masuala ya Wanawake na ulinzi wa Amani nchini, Jijini Dodoma tarehe 27/10/2021.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amefungua kikao kazi cha kuandaa Mpango kazi wa Taifa wa masuala ya Amani na Usalama wa Wanawake nchini.

Kikao hicho kinachotekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la kila nchi mwananchama kuandaa Mpango kazi kwa lengo la ushiriki wa wanawake kwenye michakato ya ulinzi na usalama na kuwalinda wanawake kwenye migogoro.

Akizungumza katika kikao hicho kinafanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma, Dkt. John Jingu amesema katika utatuzi wa migogoro, wanawake wana nafasi kubwa hivyo, azimio hilo lilikuwa ni Mapinduzi makubwa kwa kutambua kuwa kwenye migogoro kuna masuala ya kijinsia.

"Wanawake wamekuwa ni wahanga wakubwa hususani kwenye vita, unyanyasaji wa kingono hutumika kama silaha kuwaadhibu jamii nyingine ,ambapo vitendo vya ubakaji huathiri wanawake kwa kiwango kikubwa kuliko wanaume" Alisema.

"Sisi katika nchi yetu kwenye mambo yote wamekuwa wakishiriki na yamezingatiwa, lakini ili kutekeleza vizuri haya mambo lazima iundwe kikosi kazi ili kwenda pamoja," ameongeza Jingu. 

Dkt. Jingu kuwa, kama nchi na sehemu ya Jamii ya umoja wa Kitaifa lazima kutekeleza azimio hili kwa kuzingatia historia, uzoefu, taratibu na Mila na Desturi.

Aidha, ameishukuru Taasisi ya Mwl Nyerere Kwa kuungana kushiriki kutengeneza Mpango kazi huo kwani itaongeza mawazo ya uzoefu kufanikisha jambo hilo na kuwahakikishia kikosi hicho kuwa, Serikali kupitia Wizara itashiriki kikamilifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Joseph Butiku amesema jamii inatakiwa kuwaheshimu wanawake na tangu wakati wa Muungano tumetakiwa kutambua watu wote tuna haki sawa, hivyo usawa ni jambo la kuzingatia.

"Mpango kazi huu utakoandaliwa utazingatia mipango na mikakati inayoleta usawa baina ya jinsi zote ni muhimu kwa mstakabali wa maendeleo ya jamii" alisema Butiku.

Naye mshauri mbobezi wa masuala ya Sera na Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Usu Malya amesema masuala yaliyopo kwenye azimio la Umoja wa Mataifa ambayo yanalenga ushiriki wa wanawake kwenye kuzuia migogoro yatazingatiwa na Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kushirikisha wanawake kwenye nyanja nyingi ikiwemo uongozi, elimu, uchumi na migogoro hivyo Mpango kazi utaweza kuongoza vema masuala hayo kwa utaratibu mzuri.

No comments:

Post a Comment