MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo
Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo akizungumza wakati wa halfa hiyo |
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza akizungumza wakati wa Halfa hiyo
kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu
Mwana FA |
Mkurugenzi Asasi Kilele ya Sekta binafasi Tanzania Jackline Mkindi ambaye aliwakilishwa na Giliad Daniel ni Bwana Shamba kiongozi wa Asasi hiyo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya okoa mazao ya viungo Kijiji cha Kwemhosi Kata ya Nkumba kushoto ni Afisa Kilimo wa wilaya ya Muheza Hoyange Malika Mbwambo aliyakaa kushoto
Afisa Kilimo wa wilaya ya Muheza Hoyange Malika Mbwambo akieleza jambo wakati wa halfa hiyo |
KUFUATIA kuibuka kwa ugonjwa wa Mnyauko na wadudu wanaoshambulia na kuharibu mazao ya viungo wilayani Muheza waitwao Vifiripi kwenye mazao Asasi ya Sekta Binafsi Tanzania inayosimamia ukuaji endelea wa Tasnia ya ya Taha imechangia dawa ambazo zinaweza kutosheleza ekari 1000 na vitendea kazi ambavyo vitatumika kwa ajili ya kunyunyizia kwenye mashamba yao.
Akizungumza wakati kabla ya kukabidhi viwatilifu hivyo kwa Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA Mkurugenzi Asasi Kilele ya Sekta binafasi Tanzania Jackline Mkindi ambaye aliwakilishwa na Giliad Daniel ni Bwana Shamba kiongozi wa Asasi ikiwa ni uzinduzi wa kampeni ya okoa mazao ya viungo Kijiji cha Kwemhosi Kata ya Nkumba.
Giliad allisema hatua ya wao kukabidhi dawa hizo wakishirikiana na wadau wengine ikiwemo Wizara ya Kilimo, Halmashauri,Trinon na GEF ni katika kuona njia ipi rahisi ya kupambana na tatizo hilo kwa kutambua kwamba zao hilo lina mchango mkubwa kwenye fimilia.
Alisema waliamua kufanya hivyo ili kuhakikisha wanakabiliana na ugonjwa huo ili kuhakikisha wakulima wanaondokana na changamoto hizo kwa sababu zao hilo lina mchango mkubwa kwenye kijiji cha Kemhosi kata ya Nkumba,Halmashauri Muheza na Taifa kwa ujumla kwa kufanya mambo ya kimaendeleo.
“Sisi kama Taha tuliona tuna kila sababu ya kuingia na kuona namna ya kuchangia kwenye zoezi hilo kupitia Watafiti wa madawa na wadudu kuona kutumia njia ya kibailogia ili kupambana na wadudu hao na haitakupa masalia baada ya kupulizwa na ndio maana leo tumekutana “Alisema
“Sisi Taha tumechangia dawa hizo ambazo zinaweza kutosheleza ekari 1000 na vitendea kazi ambavyo vitatumika kwa ajili ya kunyunyuzia kwenye mashamba yao na tutatoa mtu ambaye atashirikiana na mabwana afya ambao watashirikiana kupilia dawa hizo”Alisema
“Lakini pia tunawashukuru wakulima waliojitokeza kuhudhuria tukio hili na wanaamini dawa hizo zitatumika kwa kufuata maelekezo ya wataalamu baada ya upuliziaji huo utasaidia kuongeza wigo wa mazao na kuendeleza wigo wa kufungua mazao yao”Alisema
Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo,Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Hoyange Malika Mbwambo alisema katika utafui ambao wameufanya wamegundua tani takribani 140 zinapoteza kwa mwaka za mavuno ya mazao hayo kutokana na uwepo wa ugonjwa huo.
Alisema hilo linatokana na ugonjwa huo wa mnyauko na wadudu wanaoitwa Vifiripi kwenye zao la Iliki na mazao hayo yanachukua nafasi ya Pili kiuchumi kwenye Halmashauri ya wilaya ya Muheza.
“Hivyo tukaona tuchukue hatua na shughuli ya leo imehusisha wadau mbalimbali wanaohusika kwenye mazao hayo na mazao hayo yanachangia kwa kiasi kikucha cha fedha kwenye Halmashauri na wakulima”Alisema
Alisema takribani Milioni 200 zinaingia kwa mwaka kwenye Mfuko wa Halmashauri kutokana na mazao hayo hivyo yanapopotea ni hasara kwa Halamshauri kwenye uchumi wake na mkulima mmoja mmoja.
Alisema hivyo walipokuwa wanajadilia kwenye mkutano wa jukwaa la mazao ya viungo walipata maelezo ya kina kuhusu mazao hayo yanavyoathirika wakaona watoe taarifa wizara ya kilimo ambayo waliunda timu na kufanya utafiti na na baadae wao wakaeleza namna ya kupata fedha kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huo.
“Hivyo Halmashauri iliona ni mzigo mkubwa hivyo kutokana na uwepo wa wadau wakaona wakashirikisha Kampuni ya Trion na kampuni ya GFP na wadau wengine walikaa chini waona na kuona namna nzuri ya kusaidia “Alisema
Naye kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwijuma alisema halmashauri ya Muheza mapato yao sio makubwa sana na ikifika mahali ambapo wanapata upungufu wa karibu milioni 200 kwenye mapato inaathiri sana kwenye mikopo ya makundi maalumu.
Alisema kwani wao kama Halmashauri wanatoa milioni 220 hivyo ukipata hasara ya milioni 200 kwenye mapato ya halamshauri inamaanisha kwamba kuna uwezekano hiyo ikiwa ni asilimia 10 itapungua kutokana na mapato kupungua kwa mapato.
“Hivyo kwanza nitoa shukurani kwa Wizara ya Kilimo, Taha kwa kuwa nasi na wadau wengine walioshirikiana nao kuhakikisha hilo linapatiwa ufumbuzi tatizo hili ambalo lilikuwa linatuumiza kichwa”Alisema
Alisema kwa sababu mapato ya halmashauri yanachangiwa na mapato ya wananchi mmoja moja kati yao wafanyabiashara na wakulima wa mazo ya viungo yaaathiri hali za maisha kama wananchi wa Nkumba na Muheza kama wameshirikiana nao ni wenzao hawatakaa wasahau mchango wao huo.
Mbunge huyo alisema miongoni mwa vitu ambayo wanaendelea kuvipigania ni kuhakikisha wanaongeza kiwango cha uzalishaji kwenye mazao ya vuungo kwa sababu wamekuwa wakipata masoko makubwa ya mazao ya viungo duniani kote na iliki ya Muheza ni nzuri kuliko maeneo mengine duniani.
Alisema lakini mtihani wanaoupata ni kwamba nazalisha kiwango kidogo hivyo ina nipa huzuni huku akitoa wito kuongeza uzalishaji kwa sababu hiyo ni vita ikiwemo kuwashukuru serikali kupitia wizara ya kilimo ambao wamewaunga mkono na kuondokana na suala la mnyauko.
Aliwataka wakulima hao hivi sasa waongeza nguvu kwenye uzalishaji kwani zao hilo linaendelea kuimrisha sambamba na kuwataka chochote kinachotokea ambacho kinapelekea kupunguza uwezo wao wa kuzalisha lazima tutoe taarifa ili kuweza kuona namna ya kuvipatia ufumbuzi jambo hilo ili kuhakikisha kilimo hakiathiri na magonjwa kama sasa.
No comments:
Post a Comment