JAMII YATAKIWA KUACHA UBAGUZI WA KIKABILA KATIKA MAHUSIANO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 5 July 2021

JAMII YATAKIWA KUACHA UBAGUZI WA KIKABILA KATIKA MAHUSIANO

Mwanaharakati na mpigania haki za Jamii, Bi. Edna Sunga akizungumza (kushoto).


JAMII
 
imeaswa kuacha vitendo vya ubaguzi wa kikabila katika mahusiano ya ndoa kwani kitendo hicho kinachangia watoto wanaozaliwa kwenye mahusiano hayo kukosa haki zao na kuishi katika mazingira magumu.

Rai hiyo imetolewa na mwanaharakati na mpigania haki za Jamii Bi Edna Sunga wakati akizungumza na wanahabari wakati akizindua kipindi Cha mtandaoni kiitwacho "Edna Sunga Connection" kitakachoruka kupitia mtandao wake wa You tube unaoitwa Edna Sunga Tv.
 
Bi Edna Sunga ambaye pia ni Mtendaji mkuu wa kampuni ya Edna Sunga Limited  alisema kwamba kufuatia vitendo hivyo vya ubaguzi katika jamii ameamua kuanzisha kipindi hicho ikiwa lengo ni kutoa elimu pamoja na kusaidia makundi mbalimbali yenye vipaji na uhitaji.

"Mimi mwenyewe ni mhanga nimeachika kwenye ndoa yangu kutokana na ndugu wa mwanaume wangu kumkataa mtoto wangu Lisa Brown kwa madai kuwa mtoto huyu nimezaa na mhindi hivyo hastahili kuwa katika kabila la wanyakyusa" alisema Edna kwa masikitiko makubwa.

Aidha alisema kwamba kupitia kipindi hicho kitasaidia kuwaunganisha wanandoa,kuibua vipaji kwa vijana ambao wanaweza kufanya vitu tofauti lakini hawana msaada wa kufikia malengo yao.

"Naiomba jamii yenye changamoto  ifuatilie kipindi hiki kupitia you tube yangu Edna Sunga Tv ili wasidiwe na kuondoa changamoto zinazowakumba " alisema.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo ambaye ni kada wa chama Cha Mapinduzi kuanzisha kipindi hicho ili kuweza kusaidia makundi mbalimbali katika jamii ambayo yanamigogoro mbalimbali yakimahusiano ya ndoa pamoja na kuishi katika mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment