Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Klabu za afya 'NMB Healthcare Club uliofanyka jijini Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifelo Sichwale, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Klabu za afya 'NMB Healthcare Club. |
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Klabu za afya 'NMB Healthcare Club uliofanyka jijini Dar es Salaam. |
BENKI ya NMB, imekuwa ya kwanza nchini kuzindua Klabu za Afya 'NMB Healthcare Club,' mtandao unaowapa wadau wa Sekta ya Afya mikopo ya vifaa kazi, mitaji na uwekezaji, huduma inayokuja huku benki hiyo ikiwa imetumia zaidi ya Sh. Bilioni 32 kutoa mikopo kwa Sekta Binafsi ya Afya, kati ya Sh. Bilioni 112.5 ilizopanga kutumia hadi mwaka 2025.
NMB Healthcare Club imezinduliwa sambamba na Kongamano la Afya 'Tanzania Health Summit 2021,' uzinduzi uliowakutanisha wadau wa Sekta ya Afya zaidi ya 150, wakiwemo madaktari, wamafasia, wamiliki wa hospitali, zahanati, vituo na vyuo mbalimbali vya afya na viongozi wa vyama washirika.
Uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ambako Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifelo Sichwale, aliipongeza NMB kwa kuwaunganisha na kuwapa uwezeshaji wadau muhimu wa Sekta ya Afya nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dk. Sichwale alibainisha kuwa, uzinduzi wa Klabu hiyo una baraka zote za Serikali na wanawaunga mkono NMB kwa juhudi zeo za kuwaunganisha Madaktari na wadau wengine muhimu wa Sekta ya Afya hapa nchini.
Dk. Sichwale aliipongeza NMB sio tu kwa kuwaunganisha wadau hao muhimu, bali utayari wao wa kutoa bure elimu juu ya fedha ambayo mahali pengine wangeipata kwa gharama kubwa, hasa inayohusu; uwekaji akiba, uwekezaji, umuhimu wa kupitisha fedha zao kwenye akaunti ya benki, pamoja na huduma zinginezo zitolewazo na NMB.
Naye Kaimu Afisa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, aliwapongeza wadau wa Sekta ya Afya kwa kuona umuhimu wa Klabu hiyo na kuwaasa ambao bado hajajiung kufanya hivyo.
Aidha alibainisha kuwa NMB imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya afya, ambako wanatoa misaada ya vifaa tiba, vikiwamo vinavyolenga kuhudumia eneo lenye changamoto nyingi, la afya ya uzazi. Aliongezea kuwa, NMB imeingia kwa nguvu moja kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wote, ambapo kupitia huduma ya Asset Financing - inayotoa mikopo nafuu mahsusi kwa Sekta Binafsi ya Afya,ambapo walitumia zaidi ya Sh. Bilioni 32 kufikia Machi mwaka huu, kati ya Sh. Bilioni 112.5 walizopanga kutumia hadi mwaka 2025.
NMB Healthcare Club ni uthubutu mwingine kutoka NMB unaowapa nguvu za ziada wawekezaji na wadau muhimu waliopo katika sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment