KUNDO: TATUENI CHANGAMOTO YA MAWASILIANO MIPAKANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 15 January 2021

KUNDO: TATUENI CHANGAMOTO YA MAWASILIANO MIPAKANI

 Kutoka kulia ni Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Kundo Mathew na kulia kwake ni Jan Kaaya wakiwa na viongozi wakielekezana namna ya kufanya kazi kwa uadilifu.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido akitoa ufafanuzi juu ya tatizo la mitando katika wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari alipokuwa kwenye ziara ya kikazi.

Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Jan kaaya akitoa ufafanuzi juu ya muingiliano wa mitandao ya kenya na Tanzania katika wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Kundo Mathew akikagua hali ya Mawasiliano katika simu wilayani Longido na upatikanaji wa  mtandao pamoja na Kuona changamoto za rooming.

Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Kundo Mathew akikagua mitambo wa Mawasiliano, hali ya mawasiliano wilaya ya Longido, upatikanaji wa mitandao ya simu mpakani Namanga.


Na Vero Ignatus, Arusha

NAIBU waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Kundo Mathew ameviomba vyombo vinavyosimamia mawasiliano kutatua changamoto za mitandao ya simu mipakani. 

Ameyazungumza hayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilayani Longido, ambapo kuna mwingiliano wa mitandao ya nchi ya jirani, tatizo ambalo wananchi wamekuwa wakililalamikia kwa muda mrefu. 

Sambamba na hayo mhe. Kundo Mathew amewataka wafanyakazi wa mashirika na makampuni ya mawasiliano, kuhakikisha wanafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa ,pindi atakapo baini uzembe miongoni mwao Wizara itafanya mamuzi ya kuwaondoa katika nafasi zao. 

Kwa upande wake  Kaimu mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Jan Kaaya amesema kuwa, wamefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la mawasilino kwa kuanza kuwepo kwa kituo cha radio ya TBC wilaya ya Longido, na kupunguza changamoto ya mito mitandao ya simu kwa kujenga minara katika wilaya hiyo.

Kaaya amesema TCRA imekuwa ikitangaza nafasi za masafa katika maeneo hayo, hivyo ametoa wito kwa jamii na Taasisi mbalimbali kwa kuwataka  kuuanzisha vituo vya radio katika maeneo hayo ili kupata taarifa za ndani na kupunguza changamoto za mawasiliano.

Aidha aliendelea kusema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA ), na Ile ya Kenya na Uganda lipo Jambo wanapolifanya kwa pamoja, ili kuhakikisha maeneo ya mpakani kote, wanapunguza kwa kiwango kikubwa Rooming ,ambayo husababisha mteja  aliyepo katika nchi hizo achajiwe na mtoa huduma wa nchi nyingine ya jirani.

"Tunaendelea kutoa Elimu kwa wananchi wetu kwamba achague mtoa huduma manually na siyo automatic ili kuepuka gharama zaidi za mawasiliano.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Dkt. Juma Mhina amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni kukosa mawasiliano, haswa wanapofika mpaka wa Namanga, hivyo amemuomba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari, kuwasaidia namna ya kuwajengea minara yenye uwezo mkubwa ili kuweze kuwa na mawasiliano yasiyokuwa na mwingiliano.

No comments:

Post a Comment