Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Derick Lugemala akitoa salamu kutoka
TADB wakati wa mkutano wadau wa Mkonge uliongozwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Mkoani Tanga. wa kwanza kulia anayefuatia kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa kulia akigawa mbegu ya Mkonge kwa mmoja wa wakulima za zao hilo mkoani Tanga Elizaberth Marandu wakati alipozindua zoezi la ugawaji wa Mbegu katika Kituo cha Taasisi ya Utafiti Tari Mlingano wilayani Muheza Mkoani Tanga wakati wa ziara yake.
BENKI ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa mikopo yenye zaidi ya thamani ya Bilioni 200 kwenye sekta ya kilimo hapa nchini ili kuongeza tija na maendeleo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao mbalimbali nchini.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Derick Lugemala wakati akitoa salamu kutoka TADB wakati wa mkutano wadau wa Mkonge uliongozwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Mkoani Tanga.
Akizungumzia TADB katika zao la Mkonge, Alisema kwamba wanaamini zao la mkonge na mazao mengine ya kimkakati ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda na uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa.
"TADB ipo kwaajili yakuhakikisha wakulima wanawezeshwa ilikubadili kilimo chetu kuwa kilimo biashara".
Aidha alisema katika mikopo hiyo walioitoa kwa mkoa wa Tanga pekee wametoa mikopo yenye thamani ya Bilioni 12 huku vyama vya msingi AMCOs na wakulima wa mkonge wakipata mikopo yenye thamani ya zaidi ya billioni 1 katika juhudi zakuwezesha kilimo cha Mkonge nchini. .
“Kwa mara ya kwanza wakati tunaliongelea zao la mkonge tulikuwa tunafikiria tutapata wapi mbegu kwa sababu ilikuwa ni shauku yetu kubwa kuongeza uwekezaji kwenye zao hilo na tulipofika tulikwenda moja kwa moja kuwatembelea watu wa TARI.
Katika hatua za awali za ushirikiano wa TARI na TADB, kwanza ilibidi tuwezesha TARI kwa kuwajengea kitalu kwa ajili ya kutengeneza mbegu na miche bora”Alisema
Nia ya TADB katika ushirikiano huu ilikuwa kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora zitakazowawezesha kupata mazao bora zaidi.
"Shauku yetu ilikuwa tukienda kwa wakulima tukiwaambia waendelee kulima mkonge tayari tulinajua wapi watapata mbegu kipekee tunawapongeza TARI kwa uwekezaji mkubwa walioufanya hapa". Alisema.
Mkurugenzi huyo wa fedha alisema wanaamini mbegu ambazo zimezalishwa wao watakuwa sehemu kubwa ya kwenda kuwakopesha wakulima waweze kununua mbegu na kuweza kupanua mashamba yao.
“Labda kwa kulipokea hilo Mh Waziri Mkuu niweze kutoa hamasa hata kwa wale ambao wanatarajia kutengeneza kitalu cha kulima mbegu hizo waweze kuona namna kuwasaliana nasi waweze kupata mikopo kutokana na kwamba bado kuna uhitaji mkubwa wa mbegu”Alisema
Hata hivyo alisema benki hiyo imeweza kuwekeza mikopo mingi kwenye sekta ya kilimo ili kuweza kuhakikisha wakulima wanalima kwa tija kubwa na kuweza kunufaika kupitia kilimo.
“Tokea tumeanza kazi ya kuchochea upatikanaji wa mikopo kwenye sekta ya kilimo mwaka 2016 mikopo iliyokwenda kwenye sekta ya Kilimo ilikuwa kwa asilimia 85 ilikuwa ni ongezeko kubwa sana”Alisema
Aliongeza kuwa TADB kwa kuona wakulima wengi hawakopesheki kwenye taasisi nyingi za kifedha kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo, TADB imeingia ushirika na taasisi za kifedha 11 na kutoa dhamana kwa wakulima.
Katika zao la Mkonge tumewezesha vyama vya msingi, kampuni na wakulima binafsi kupata mikopo kwenye taasisi zingine za kifedha kupitia mfuko huo wa dhamana.
“Tunamshukuru Rais Dkt John Magufuli na wewe Mhe. Waziri Mkuu, Wizara zote na wadau mbalimbali ambao tumekuwa tukifanya kazi pamoja kuchochea uwekezaji endelevu kwenye sekta ya kilimo nchini”Alisema
Ambapo Jumla ya Tsh Bilioni 1 za dhamana zimetolewa na TADB kupitia benki Washirika kama vile TPB,CRDB na NMB.
No comments:
Post a Comment