Wananchi
wa Kijiji cha Bweni wilayani Pangani ambacho kimefanya vizuri katika
Shindano ya Mapambano
dhidi ya Ukatili wa Kijinsia zidi ya Wanawake na Watoto wakiwa na tuzo
yao huku wakisheherekea baada ya kuibuka na ushindi wa Vijiji ambavyo
vimefanya vizuri katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto
wilayani Pangani.
Wananchi wa Kijiji cha Bweni wilayani Pangani ambacho kimefanya vizuri
katika Shindano ya Mapambano
dhidi ya Ukatili wa Kijinsia zidi ya Wanawake na Watoto wakiwa na tuzo
yao huku wakisheherekea baada ya kuibuka na ushindi wa Vijiji ambavyo
vimefanya vizuri katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto
wilayani Pangani.
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange kulia akitoa tuzo kwa mmoja wa viongozi wa vijiji vilivyofanya vizuri katika mapambano dhidi ya ukatili
wa wanawake na Watoto wilayani humo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange
akizungumza mjini humo wakati wa tamasha la kuwazawadiwa vijiji
bora katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani humo
lililoendeshwa na Shirika la Uzikwasa wilayani humo kulia ni Mkurugenzi
wa Uzikwasa
Novatus Urassa.
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange
akizungumza mjini humo wakati wa tamasha la kuwazawadiwa vijiji
bora katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani humo
lililoendeshwa na Shirika la Uzikwasa wilayani humo kulia ni Mkurugenzi
wa Uzikwasa
Novatus Urassa.
SERIKALI wilayani Pangani mkoani Tanga imeitaka jamii
kutoyaficha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na Watoto
kwani kwa kufanya hivyo wanachangia kurudisha nyuma jitihada za
maendeleo katika Taifa.
Ushauri
huo umetolewa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mwalimu Hassani Nyange wakati wa tamasha la
kizawadia Vijiji vilivyofanya vizuri katika mapambano dhidi ya ukatili
wa wanawake na Watoto wilayani humo.
Alisema
Kuwa swala la ukatili wa kijinsia katika jamii ni tatizo ambalo Kama
halitatolewa taarifa na hatua za kisheria kuchukuwa mkondo wake
litaendelea kuleta athari zaidi .
"Hivi
vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto wadogo Kama kubakwa na
kulatiwi ndio ikiwa havitadhibitiwa kwa haraka vitaweza kuleta athari
zaidi kwa watoto hao ambao ni Taifa la kesho"alisema DAS Nyange.
Nae
Mratibu wa tamasha hilo kutoka Shirika la Uzikwasa Salvata Katanga
alisema kuwa Shirika hilo limekuwa likiwazawadia tuzo Vijiji kumi
ambavyo vinafanya juhudi kubwa katika kupinga mapambano dhidi ya ukatili
wa kijinsia wilayani humo.
Alisema
kuwa tamasha hilo limeweza kusaidia viongozi wa Vijiji husika kuwa
wabunifu katika kudhibiti vitendo vya ujanyanyasaji kwa kutoa taarifa
mapema katika vyombo vya usalama na hatua kuchukuliwa.
Kwa
upande wao baadhi ya viongozi wa Vijiji walisema kuwa elimu
waliyoipata imewezesha kusaidia kuishirikisha jamii katika utekelezaji
wa mpango Kazi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.
Mwenyekiti
wa Kijiji Cha Mkwaja Saleh Mwinjuma alisema kuwa wamefanikiwa kutoa
elimu ya athari za ukatili na namna ya kuripoti matukio hayo kwenye
vyombo vya kisheria
"Elimu
imesaidia kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia kwani hapoa awali
wananchi walikuwa wanaogopa kutoa taarifa lakini baada ya kupata elimu
sasa jamii imehamasika kutoa taarifa hizo"alisema Mwinjuma.
Nae
Mwakilishi wa dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi Ismail Ali alisema
kuwa kutoka na jamii kuhamasika hivi karibuni waliweza kupa taarifa ya
matukio ya watoto kulawitiwa na waliweza kufanikiwa kuwatia nguvuni
wahusika.
"Hivi karibuni
tulipata taarifa ya watoto watano kulawitiwa katika kata ya Boza na
kutokana na ushirikiano wa jamii tuliweza kuwatia nguvuni wahusika na
Sasa wanatarajia kufikishwa Mahakama wakati wowote,"alisema Ali.
No comments:
Post a Comment