MWENYEKITI WA TUME AWATAKA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 17 October 2020

MWENYEKITI WA TUME AWATAKA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU

 

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (mst) Semistocles Kaijage akifungua mkutano wa Watendaji wa Uchaguzi Mkoa wa Dar es Salaam. Jaji Kaijage amewataka watendaji hao kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha kwamba kwenye Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, Sheria, Kanuni na Taratibu zinafuatwa.

Mkutano huo uliwaleta pamoja Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa, Maafisa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata. Mkutano kama huo umefanyika kwenye vituo saba (7) nchi nzima.

Mkutano wa Watendaji wa Uchaguzi Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na NEC ukiendelea.

Mkutano wa Watendaji wa Uchaguzi Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na NEC ukiendelea.

No comments:

Post a Comment