Mwenyekiti wa kamati inayoratibu tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tazania kutoka kwa wazee na jamii ya watu wa mkoa wa Kilimanjaro,Yunusi Mmari akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi kilichofanyika katika ukumbi wa Kili Home mjini Moshi.
Katibu wa kamati ya maandalizi ya tukio hilo Joseph Msele akizungumza katika tukio hilo.
Mzee Akili Kawishe akifurahia jambo na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho.
Mzee Akili Pendael Kawishe ni mzee mwenye umri wa miaka 102 akiwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tukio hilo Yunusi Mmari wakati wa kikao kilichofanyika mjini Moshi.
Baadhi ya Vikundi vya ngoma za asili vikionesha namna vilivyoanza maandalizi kwa ajili ya tukio hilo linalotaraji kufanyika mwezi ujao mkoani Kilimanjaro.
Na Dixo Busagaga, Moshi
WAZEE katika mkoa wa
Kilimanjaro wakiwemo viongozi wa Mila, Machifu na Malaigwanani wameanza
mchakato wa kumpongeza na kumpa Tuzo Maalumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kazi aliyofanya katika kipindi cha miaka mitano.
Katika tukio hilo
wananchi wenye asili ya kanda ya kaskazini wanakusudia pia kumuomba radhi Rais
Magufuli kutokana na maamuzi waliyofanya wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
kwa kumpa kura chache.
Mwenyekiti wa kamati
inayoratibu tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania kutoka kwa wazee na
jamii ya watu wa mkoa wa Kilimanjaro, Yunusi Mmari alisema maandalizi ya tukio
hilo tayari yameaza huku yakishirikisha wazee kutoka wilaya zote za mkoa wa
Kilimanjaro.
“Kusudio la tukio hili
ni kuwakutanisha Wazee kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani
wakiwemo Wazee wa mila kama Machifu na Malaigwanani ambao watakuwa na ujumbe
maalumu wanaotarajia kuufikisha kwa Rais Dkt Magufuli,” alisema Mmari.
Kwa upande wake katibu
wa tukio hilo Joseph Msele alisema watu wengi wamejiandaa kushiriki huku kamati
kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali vikiangalia eneo kubwa zaidi la
kufanyika kwa tukio hilo.
“Watu wengi
wamejiandaa kushiriki katika tukio hilo, tulikua tunafikiria kulifanyia uwanja
wa Ushirika lakini kwa hesabu ambazo mpaka sasa tunazo tunaona uwanja wa
ushirika mpaka sasa umejaa, hautoshi.
“Tunaendelea
kuwasiliana na vyombo husika ili kuweza kuona ni eneo gani walau linaweza
likakidhi hiyo population inayotarajiwa ni watu wengi san asana, wanasubiri kwa
hamu.” aliongeza Msele.
Kuhusu Shauku ya watu
wa Kanda ya Kaskazini kuonana na Rais Magufuli, Msele alisema: “Ni kweli imekua kiu
ya wengi kutamani kumpatia Mh Rais Dk. John Pombe Magufuli tuzo na sisi kazi
yetu kama kamati ni kuratibu tu hayo mawazo ya wengi ili kuyafikisha kwenye
kilele hicho,” alisema Msele.
Alisema wapo wazee wenye
umri zaidi ya miaka 100 wao pia wamekuwa
na shauku ya kumpongeza Rais, Dk. Magufuli huku akitoa rai kwa vyombo vya
usafiri yakiwemo Mabasi, Treni, Ndege kujipanga kusafirisha wakazi wa mikoa ya
kaskazini kuhudhuria tukio hilo.
“Niwaombe pia viongozi
wa taasisi mbalimbali za kiserikali na ambazo sio za kiserikali wawaruhusu
wakazi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wahudhurie tukio hili watakapo pata
taarifa ya tukio hili ,” alisema Msele.
Miongoni mwa Machifu
walioshiriki katika kikao cha maandalizi ni pamoja na Mangi Frank Mareale
pamoja na Akili Pendael Kawishe mzee wa miaka 102 wakazungumzia juu ya tukio
hilo.
Tukio la Pongezi na
utoaji tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
linataraji kupambwa na vikundi vya ngoma za asili ambavyo vimekuwa sehemu ya maandalizi ya tukio hilo.
No comments:
Post a Comment