TTCL YAHUDUMIA ZAIDI YA WATEJA 2200 MAONESHO YA SABASABA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 13 July 2020

TTCL YAHUDUMIA ZAIDI YA WATEJA 2200 MAONESHO YA SABASABA

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bi Regine Hess (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhusu moja ya huduma ya internet inayotolewa na shirika hilo, alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Uhusiano wa TTCL, Bi. Puyo Nzalayaimisi akifuatilia.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bi Regine Hess (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa TTCL, Bi. Puyo Nzalayaimisi (wa pili kulia) alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakipata huduma mbalimbali walipotembelea Banda la TTCL katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakipata huduma mbalimbali walipotembelea Banda la TTCL katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakipata huduma mbalimbali walipotembelea Banda la TTCL katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

BANDA la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetoa huduma kwa zaidi ya wateja 2220 waliotembelea kupata huduma anuai kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yaliomalizika leo Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kufungwa rasmi kwa maonesho hayo leo, Meneja wa Banda la TTCL ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa TTCL, Bi. Puyo Nzalayaimisi amesema zaidi ya wateja 2220 wamehudumiwa kwa huduma mbalimbali katika maonesho, ukiachilia Watanzania wengine waliofika kutazama huduma na bidhaa walizozileta katika maonesho hayo.

Meneja huyo alisema, wanawashukuru wateja na Watanzania wote waliotembelea kupata huduma mbalimbali katika banda lao kwenye maonesho ya mwaka huu, na TTCL itaendelea kutoa huduma bora na nafuu kwa Watanzania kwani linatambua na kujali mchango wao. 

"...Kipekee napenda niwashukuru sana wateja wetu na Watanzania wengine waliotutembelea katika Banda letu kwenye maonesho ya mwaka huu, TTCL itaendelea kuwahudumia vizuri popote," alisema Bi. Puyo Nzalayaimisi akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Aidha aliwakumbusha wateja kuendelea kujipatia huduma ya T-Burudani nyenye ofa kwa sasa ambayo kwa shilingi 2000 inampa mteja GB 1 ya kuangalia na kupakua filamu na tamthilia aipendayo kwa siku nne.


Miongoni mwa huduma ambazo TTCL ilikuwa ikizitoa katika banda lao ni pamoja na huduma za usajili laini kwa wateja, kurudisha laini zilizopotea,vifaa vya internet kama modem na vinginevyo, huduma za T-PESA, huduma za mkongo wa taifa wa mawasiliano na huduma za Data Senta.

No comments:

Post a Comment